Connect with us

International Football

RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA HISPANIA AACHIA NGAZI.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Hispania Luis Rubiales mapema leo amewasilisha barua ya kujihudhuru wadhifa wake kwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Pedro Rocha kutokana na mashinikizo yaliyokuwa yakimtaka aachie ngazi baada ya tukio la kumbusu mchezaji wa timu ya Taifa ya Hispania Jennie Hermeso.

“siwezi kuendelea na kazi”

Alisema Luis Rubiales Rais wa Shirikisho la Soka Hispania.

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) lilikuwa likimshinikiza wakati wote Rubiales kuachia ngazi lakini pia wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake walikataa kuitumikia timu hiyo hadi pale kiongozi huyo atakapokubali kuachia ngazi, awali Mama mzazi wa Luis alikataa kula na kujifungia kanisani kutokana na kile mwanae anachokipitia.

kwasasa kinachosubiriwa ni majibu ya barua aliyoituma Rais huyo kwa Shirikisho la Soka Hispania.

Rubiales alitenda tukio la kumbusu mchezaji huyo katika fainali za kombe la Dunia kwa wanawake zilizofanyika mapema mwaka huu baada ya timu yake kuibuka mabingwa mbele ya Uingereza waliposhinda goli 1-0 katika mchezo wa fainali.

Makala Nyingine

More in International Football