Connect with us

Michezo Mingine

DAR CITY AU JKT NANI KUWA MBABE WA KIKAPU DAR?

Ligi ya mchezo wa Mpira wa Kikapu ya jijini Dar Es Salaam(BDL) inafikia tamati kwa kuwakutanisha wababe wawili Dar City na JKT baada ya kuwatoa ABC na PAZI kwenye michezo ya playoffs ya nusu fainali.

Mchezo huu wa Fainali unatarajiwa kuwa wa mechi 5(Best of 5) na mchezo wa kwanza utapigwa Jumamosi tarehe 23/09/2023 majira ya 1.30 jioni kwenye uwanja wa Don Bosco, Oysterbay.

Daudasports Tutakuwa nawe bega kwa bega kukujuza matokeo ya Fainali hii kali kabisa. Macho yatakuwa kwa Ally Faraj wa Dar City na Baraka wa JKT, nani kuwa MVP?

Makala Nyingine

More in Michezo Mingine