Connect with us

International Football

SIMBA YAELEKEA NDOLA NA 24, KRAMO OUT

Aubin Kramo(Kushoto) akiwa na Che Malone Fondoh Mazoezini

Klabu ya soka ya Simba Sports Club imesafiri leo kuelekea jijini Ndola, Zambia kwa ajili ya mchezo wao wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power Dynamos ya nchini humo katika mchezo wa utangulizi wa pili kuelekea hatua ya makundi ikiwa na msafara wa Viongozi na wachezaji 24 huku nyota kutoka Ivory Coast, Aubin Kramo Kouame akikosekana kwenye msafara huo.

Kramo, alipata majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Ngome Fc ya Dar Es Salaam kwenye ushindi wa 6-0 wakati akifunga bao lake la 3 kwenye michezo yote ya kirafiki aliyocheza akitokea kwenye majeruhi(dhidi ya Kipanga, Cosmopolitan,Ngome FC) na kummlazimu kutolewa nje baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.

Taarifa juu ya majeraha yake zinasema kuwa atakuwa nje kwa muda huku huenda ikalazimu kufanyiwa upasuaji. Wachezaji wengine wanaokosekana kwenye msafara huu ni pamoja na Nassoro Kapama, Mohamed Mussa na Ferooz.

Kikosi kamili kilichosafiri kinawajumuisha, Magolikipa Ally Salim, Hussein Abel na Ayoub Lakred. Walinzi ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, David Kameta, Israel Mwenda, Henock Inonga Baka, Che Fondoh Malone, Hussein Kazi na Kennedy Juma.

Viungo ni Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma, Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama, Luis Miquissone, Willy Essomba Onana, Kibu Dennis na Hamis Abdallah.

Washambuliaji ni Jean Baleke, Patrick Phiri, Shabaan Iddy Chilunda na Nahodha John Bocco.

Mchezo unatarajiwa kupigwa Jumamosi ya tarehe 16/09/2023 majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania kwenye dimba la Levy Mwanawasa.

Makala Nyingine

More in International Football