Connect with us

EPL

Hannibal Kuongezewa Mkataba Mrefu

Hannibal Mejbri

Klabu ya Soka ya Manchester United ya Uingereza haina presha ya kummbakisha kijana wao raia wa Tunisia, Hannibal Mejbri, 20, kikosini licha ya mkataba wake kuelekea ukingoni.

Manchester United wanaamini sio jambo la haraka sana kwani bado wana kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi mkononi mwao lakini wanaamini kuwa ipo haja ya kufanya nae mazungumzo juu ya mkataba mrefu zaidi.

Hannibal amefanikiwa kummshawishi kocha Ten Hag kummpanga kama kiungo msaidizi wa Nahodha Bruno Fernandes mbele ya wakongwe kama Donny Van De Beek na kwenye michezo miwili iliyopita ameweza kuonyesha kwanini ameaminiwa akicheza vizuri michezo yote na akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Brighton, United wakipoteza 3-1.

Makala Nyingine

More in EPL