Connect with us

NBC Premier League

REKODI ZA LIGI KUU MZUNGUKO WA TANO

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ipo mzunguko wa tano na kila timu imecheza michezo mitano.

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara iko mzunguko wa tano hivi sasa ikiwa kila timu imecheza michezo mitano (5), hii ni taarifa fupi ya kilichoendelea hadi kufikia mzunguko wa Tano.

Klabu ya Simba na Azam ndio pekee ambazo hazichapoteza mchezo wowote katika michezo mitano (5) waliyocheza. Simba imevuna alama kumi na tano (15) na ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu Kandanda Tanzania Bara na Azam ikiwa nafasi ya pili ya msimamo na alama kumi na tatu (13).

Klabu ya Mashujaa yenye maskani yake mkoani Kigoma hadi kufikia mzunguko huu wa tano (5) ndio klabu pekee iliyofungwa magoli machache (1) kuliko klabu yoyote ile, walinda lango Lameck Kanyonga na Hashimu Mussa wa klabu hiyo kila mmoja ana cleansheet mbili (2).

Vinara wa cleansheet hadi hivi sasa ni Djigui Diarra wa Young Africans na Idrissu wa Azam fc wenye cleansheet tatu (3) kila mmoja.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League