Connect with us

Simba

SIMBA SC NA ATCL BADO KUENDELEA KUFANYA KAZI PAMOJA

ATCL inafurahi sana kuwa mbia wa Simba na iko tayari kufanya kazi pamoja na Simba katika kusafirisha timu na pia mashabiki

Klabu ya Simba imethibitisha kuendeleza ushirikiano na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) rasmi ACTL imekubali kuendelea kuipa Simba fursa ya kutumia huduma za ATCL kwenye safari za klabu hiyo.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kuishukuru ATCL kwa uhusiano mzuri na Simba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema.

“ATCL mmekuwa washirika muhimu sana kwenye mafanikio ya Klabu ya Simba kwa kutupa usafiri wa uhakika na bora kwa ajili ya timu yetu. Tukielekea kwenye mechi ya AFL dhidi ya Al-Ahly tufurahi kujua kwamba ATCL itakuwa mbia muhimu kusafirisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali kuja kuangalia mchezo huo.”

“ATCL inafurahi sana kuwa mbia wa Simba na iko tayari kufanya kazi pamoja na Simba katika kusafirisha timu na pia mashabiki.”

Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Jamal Athuman Kiggundu.

Makala Nyingine

More in Simba