Connect with us

Makala Nyingine

LIGI YA SOKA LA UFUKWENI ITANIPA TIMU BORA COSAFA-PAWASSA

Kocha wa timu ya taifa ya soka la ufukweni, Boniphace Pawassa amesema kuwa anaridhishwa na mwenendo wa ligi ya mchezo huo kwani anaona maendeleo makubwa katika uchezaji kutoka kwa wachezaji wa timu shiriki na anaona atapata timu bora sana kuelekea michuano inayofuata ya timu ya taifa ikiwemo mashindano ya COSAFA.

Kiukweli kabisa naona maendeleo makubwa kwa wachezaji wengi niliokuwa nikiwafuatilia na naona kabisa nitakuwa na timu nzuri sana kuelekea kwenye mashindano yaliyo mbele yetu.

Unajua mwezi ujao(Novemba) kuna mashindano ya COSAFA yatafanyika Durban, South Afrika na huwa tunaenda kushiriki na hayako mbali hivyo kupitia ligi hii naona kabisa nitapata timu imara lakini pia hata kwenye mashindano ya Copa Dar mwezi wa 12.

Pawassa pia hakusita kuwasihii wadhamini na wadau kujitokeza kuunga mkono mchezo wa soka la ufukweni kwani unaweza kuitangaza zaidi pia Tanzania kimataifa na ni mchezo unaokuwa kwa kasi.

Tunawashukuru sana wadau wanaoendelea kutushika mkono kwenye ligi lakini bado tunatafuta wadhamini zaidi. Kwa mfano kwenye Copa Dar, tuanatafuta bado wadhamini wa michuano hii ili izidi kuwa bora na inafanyikaga kila Disemba ya kila mwaka na inashirikishaga timu nyingi za kigeni pia.

Ligi ya soka la ufukweni inatarajiwa kuingia kwenye mzunguko wake wa 6 wikiendi hii ambapo Jumamosi zitachezwa mechi 4 za kundi B na Jumapili zitachezwa mechi zingine 4 za kundi A, kwenye fukwe za Coco kuanzia saa 6 Mchana.

Timu shiriki zipo 16 na zimegawanywa kwenye makundi mawili A na B kwa timu 8 kila kundi.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine