Tanzania kwa mara ya kwanza ilifuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980, zilizokuwa zikifanyika Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho zilikuwa zikishiriki timu nane pekee. Taifa Stars ilipata tiketi ya kushiriki michuano hii baada ya kuiondosha timu ya Taifa ya Zambia mwaka 1979 kwa jumla ya goli 2-1, katika mchezo wa kwanza Tanzania iliibuka na ushindi wa goli 1-0, na katika mchezo wa marejeano uliopigwa August 26, 1979 pale ndola, Zambia Tanzania ililazimisha sare ya 1-1, mbele ya Rais wa nchi hiyo Keneth Kaunda ambaye alitoa ahadi ya gari na nyumba kwa kila mchezaji iwapo watafuzu AFCON 1980 kwa kuiondosha Tanzania.
Hiyo ikawa Makala ya kwanza kwa Tanzania kufuzu kwenye Fainali za AFCON, kwa kipindi hicho timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa ikiundwa na nyota kama Juma Pondamali Mensah, Leonard Taso, Mohamed Kajole, Leodgar Tenga, Gela Mtagwa, Juma Makumbi, Omary Hussein, Hussein Ngulungu, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni Ally, goli la Tanzania lilifungwa na Peter Tino na goli pekee la Zambia lilifungwa na Alex Cholla aliyekuwa anacheza mabingwa Afrika kwa kipindi kile Mfulira Wonderers.
Timu hizi mbili zimepangwa kundi moja (KUNDI F) hivyo zitakutana tena kwenye Makala ya 34 ya fainali za mataifa ya Africa ( AFCON 2023) zitakazofanyika nchini Ivory Coast, ikiwa kwa Tanzania ni Makala zake za tatu kushiriki kwenye mashindano haya, huku Zambia ikiwa ni Makala yake ya 19 na wana historia ya kuwa mabingwa wa Afrika mwaka 2012, mara hii Stars itakuwa ikiundwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya Tanzania kama ilivyo pia kwa Zambia.
Upekee wa mchezo huu unabebwa na wachezaji wengi kufahamiana Zaidi, ambapo wengine wanacheza Ligi moja kama ilivyo kwa Kennedy Musonda [Yanga] na Clatous Chama [Simba], kama hawa watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea Ivory Coast na timu ya Taifa ya Zambia basi itakuwa ni mechi yenye ushindani wa aina yake. Katika michezo minne ya hivi karibuni ambayo timu hizi zimekutana Tanzania haijawahi kupata ushindi, imetoa sare moja [1] na kupoteza tatu [3].
Mchezo mwingine kwa Tanzania ambao unatazamwa kuwa na ushindani kwnye kundi F ni dhidi ya DRC ambapo baadhi ya nyota wa kikosi hicho wanacheza Ligi kuu Tanzania Bara kama Henock Inonga anayekipiga ndani ya klabu ya Simba na Fiston Mayele aliyewahi kucheza Young Africans.
Mchezo unaotazamwa kuwa mgumu zaidi kwa Tanzania ni dhidi ya Morocco, timu ambayo ilimaliza nafasi ya nne kwenye fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar, kwani timu hii ina nyota wengi kama Achraf Hakimi anayekipiga PSG na Sofyan Amrabat anayekipiga Manchester United.
Je, Tanzania itaenda kuvunja historia nyingine kwenye fainali za mataifa ya Afrika 2023 nchini Ivory Coast mbele ya Zambia ?
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...