Connect with us

Makala Nyingine

IHEFU KUTANGAZA KOCHA MPYA.

Klabu ya Ihefu imepanga kumtangaza kocha wake mpya kabla ya mchezo dhidi ya Coastal Union October 21.

Klabu ya Ihefu baada ya kutangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Zuberi Katwila kwa makubaliano ya pande zote mbili, kupitia kwa Afisa habari wake Peter Andrew imesema kwasasa inafanya upembuzi na uchambuzi wa kina wa kujua ni nani atakuja kuendeleza gurudumu lililoachwa na Zuberi Katwila.

Dunia nzima ina makocha wengi sana, kwasasa tunafanya upembuzi na uchaguzi kuhusiana na mahitaji yetu, hatuwezi kuwa na presha ya kumtangaza kwa haraka kwasababu leo ndio tumetangaza kuachana na mwalimu, Tunahitaji muda kidogo wa kufanya uchunguzi ili kujua nani atakuja kuendelea pale ambapo Zuberi ameishia.

Peter Andrew, Afisa Habari Ihefu kuhusu kumtangaza kocha mpya.

Baada ya kuachana na katwila, Je Ihefu itaajiri kocha kutoka ndani ya nchi ama nje ya nchi ? Peter Andrew amesema hilo linajadiliwa na bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo ambao wao ndio wanajua.

Bodi ya wakurugenzi ndio wanaojua ni aina gani ya mwalimu ambaye wana muhitaji, kwahiyo sisi kama viongozi tumeliacha ngazi za juu zaidi ambao ndio wanaotoa maamuzi.

Peter Andrew akizungumzia kuhusu kuajiri kocha wa kigeni ama Mzawa.

Vilevile Peter Andrew amesema klabu hiyo inampango wa kutangaza kocha mpya wa kikosi hicho kabla ya mchezo wao unaofuata dhidi ya Coastal Union utakaopigwa October 21 katika dimba la Highland Estate, jijini Mbeya.

Juma hili hili lazima tutamtangaza mwalimu kwasababu tuna mechi ya Ligi hivi karibuni, hatuwezi kwenda kwenye mechi bila kocha mkuu……. mpaka kufikia mchezo wetu na Coastal Union tutakuwa tushamtangaza mwalimu.

Peter Andrew Afisa habari wa klabu ya Ihefu.

Kwa upande mwingine Peter amewataka mashabiki wa ihefu wawe wavumilivu katika kipindi hiki ambacho wanatafuta mwalimu mpya atakaekuja kuchukua nafasi iliyoachwa na mwalimu Zuberi Katwila.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine