Connect with us

NBC Premier League

IHEFU YAACHANA NA KOCHA WAKE.

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu klabu ya Ihefu itoe kichapo cha goli 2-1 kwa klabu ya Young Africans, leo imetangaza kuachana na kocha wake mkuu Zuberi Katwila aliyehudumu kikosini hapo kwa takribani miaka mitatu (3) tangu mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu ya ihefu Peter Andrew hakuweka wazi sababu za kuachana na kocha Zuberi katwila zaidi ya kusema ni makubaliano ya kimkataba baina ya pande mbili.

Zuberi Katwila ameiongoza klabu ya Ihefu msimu huu katika michezo mitano (5) akishinda michezo miwili (2) na kupoteza michezo mitatu (3) ameiacha klabu ikiwa katika nafasi ya nane (8) ya msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League