Connect with us

Taifa Stars

TANZANIA NA SUDAN KUKIPIGA LEO.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kirafiki hii leo dhidi ya Sudan saa moja kamili Jioni huko Saudi Arabia.

Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki hii leo dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan huko nchini Saud Arabia.

Mchezo huo utapigwa leo Oktoba 15 katika uwanja wa King fahd kwenye mji wa Altaif, majira ya saa 1:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Timu ya Taifa ya Tanzania itashuka Dimbani hii leo ikiongozwa na nyota kadhaa wanaocheza nje ya Tanzania akiwemo Nahodha wa kikosi hicho Mbwana Ally Samatta [Paok FC – Greece], Abdulrazack Hamza [Supersport – Afrika Kusini], Baraka Majogoro [ Chippa United – Afrika Kusini], George Mpole [saint Eloi Lupopo – DR Congo], Said Hamis [FK Jedinstvo-Serbia], Morice Abraham [FK Sportak Subotica – Serbia], Haji Mnoga [aldershot Town – England], Ben Starkie [Basford United – England], Saimon Msuva [JS Kabyle – Algeria], Novatus Miroshi [Shakhtar Donetsk – Ukraine], Abdi Banda [Richards bay – [Afrika Kusini], Himid Mao [Tala’ea El Gaish – Egypt].

Nyota wengine wanaokiunda kikosi hicho wanacheza Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ambao ni Beno Kakolanya [singida], Metacha Mnata, Nickson Kibabage,Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Mudathir Yahya, Clement Mzize [Young Africans], Ally Salim, israel Mwenda, Kibu Denis, Mzamiru Yassin [Simba], Abdul Suleiman, Sospeter Bajana [Azam], Abdulmalik Zakaria [Namungo], Nassor Saadun [Ihefu].

Makala Nyingine

More in Taifa Stars