Connect with us

Makala Nyingine

HENDERSON: INAUMIZA KUZOMEWA NA MASHABIKI WENU.

Henderson alizomewa kwenye mchezo wa England dhidi ya Australia uliomalizika kwa England kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika uwanja wa Wembley Ijumaa iliyopita.

Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya England Jordan Henderson ambaye kwasasa ana kipiga kwenye klabu ya El Ettifaq ya nchini Saudi Arabia, Ijumaa iliyopita wakati anaitumikia timu yake ya Taifa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Australia kwenye dimba la Wembley alizomewa na mashabiki wa timu hiyo alipokuwa akifanyiwa mabadiliko kumpisha Kieran Trippier. Mchezo huo ulimalizika kwa England kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililofungwa na Ollie Witkins.

Mashabiki hao walimzomea Henderson kutokana na maamuzi aliyoyachukua ya kwenda kucheza soka nchini Saudi Arabia kwenye klabu ya El Ettifaq. Jordan amesema hii inaumiza sana kuona mashabiki wenu wanakuzomea lakini yeye anaamini kila atakapopata nafasi ya kuitumikia timu hiyo atajitoa kwa moyo wote.

Kila mmoja ana maoni yake. Napenda kuichezea England, nimecheza kwa miaka mingi, na ndio maana nipo hapa. Bado nahitaji kuitumikia England kwa namna ninavyoweza na kutoa kila kitu kwaajili ya Taifa langu. Sio vizuri, mashabiki wenu wakikuzomea. Lakini sikiliza, kila mtu ana maoni yake. Lakini sikiliza, haitabadili chochote kwangu na kile ninachofanya kwa timu yangu na kwa Taifa langu.

Jardon Henderson akizungumza mara baada ya mchezo.

Kama watu wakiamua kunizomea kwasababu nacheza Taifa lingine ni sawa. Nilizungumza mwanzo sababu za mimi kucheza huko, kama watu wakiamua kutuamini au kutokutuamini hiyo ni juu yao, lakini nikiwa hapa na England, haitabadili chochote.

Henderson aliongeza.

England itashuka tena dimbani kuikabili Italy kesho Jumanne katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya EURO 2024 itakayofanyika nchini Ujerumani.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine