Dunia ya mpira wa miguu ina vitu vingi ambavyo vipo sirini na inahitaji muda kufahamu ila hakuna nchi duniani inatupa tu pesa zake bila mipango, China alikuwa na ndoto ya World Cup baada ya Project ya Chinese 2050 kufeli mbele ya Qatar ambao waliinunua PSG kimkakati na kuwekeza sana Ulaya wakaipata World Cup 2022.
FIFA wakati wanasaka Mdhamini wa michuano hii mikubwa na mipya kwa klabu Afrika walifahamu ndoto za Saudi Arabia kuhodhi World Cup 2034, ni ndoto ya Mwana Mfalme ambaye ni Waziri wa Michezo Prince AbdulAziz Bin Turki Al Faisal na Crown Prince Mohamed Bin Salma.
Haikutosha kwa Saudi Arabia kuimiliki Newcastle ya England, haitoshi kuwa wenyewe wa Klabu Bingwa dunia na kuwa na Ligi yenye Mastaa wakubwa sana pamoja wanahodhi Asian Cup 2029 lakini walihitaji kupata sapoti kutoka Mabara mengine nayo ni Afrika, ndipo mchoro huu ulipotokea.
Wakati Rais was FIFA Gianni Infantino na Rais was CAF Patrice Motsepe sambamba na Magwiji wa soka la Afrika kama Pinnick Amaju, Faouzi Lekja, walipopeleka uhitaji wa dola Million 200 basi Wizara ya Michezo kupitia bodi yao ya Utalii wakataka kufahamu watapata kile wanachokitaka? Yaani mileage na Dunia ifahamu.
CAF cha kwanza waliandaa mchoro wa klabu 16 kisha baadae zikapunguzwa mpaka nane peke, mtazamo mkubwa ni mtaji mkubwa wa Mashabiki, mandhari sahihi ya mpira wa miguu na umaarufu wa mchezo, target yao kubwa ni hii michuano kwenda duniani.
Hapakuwa na muundo maalumu wa kuzipata timu shiriki lakini kigezo cha kila kanda mwakilishi angalau mmoja ilikuwa kigezo, kisha nani mbabe kwenye kanda husika? Nani ana nguvu kwenye kanda husika? tunaweza kupata mileage tunayotaka? Maswali hayo.
Ndio maana jana tulipofika wakawa baadhi wanatuuliza huu uwanja utajaa? Majibu yalikuwa ndio, wenyewe hawana shaka na hilo ila wanataka Simba wathibitishe hilo Ijumaa, wakajaze kasri la soka la Tanzania na mechi yao na Al Ahly haijaja kwa bahati mbaya.
Ijumaa hii SIMBA ameshika karata muhimu ya SAUDIA kuelekea kombe la dunia!.