Connect with us

Azam FC

AZAM KUMSAJILI KIPA WA TABORA UNITED JANUARY.

Klabu ya Azam ina mpango wa kumuongeza kikosini Djuma Shaban na John Noble kwenye dirisha dogo la mwezi January.

Tetesi zinasema klabu ya Azam ina mpango wa kuachana na nyota wake wawili ambao majina yao hayajawekwa wazi katika dirisha dogo la mwezi January ili kupisha usajili wa mlinzi wa zamani wa Young Africans na AS Vita Djuma Shaban, nyota mwingine anayetajwa kujiunga na wana lambalamba mwezi January ni nyota wa zamani wa Enyimba ya Nigeria mlinda lango wa klabu ya Tabora United raia wa Nigeria John Noble.

Tayari Azam na Tabora United zimeshakubaliana kila kitu. Baada ya dili hilo kukamilika Tabora United itaingia sokoni kutafuta golikipa mwingine atakayechukua nafasi ya John Noble. Jicho la Tabora United lipo kwa mlinda lango wao wa zamani Ngeleka Allen Katembo raia wa DR Congo ambaye aliipandisha daraja timu hiyo. Kwasasa Katembo anaitumikia klabu ya Kagera Sugar.

Kwa mujibu wa tetesi zinasema kuwa endapo John Noble atajiunga na klabu ya Azam atalipwa TZS 21 Million ikiwa ni mara tatu zaidi ya mshahara anaolipwa kwasasa kwenye kikosi cha Tabora United. John akiwa na kikosi cha Tabora United analipwa kiasi cha TZS 7 Million na tayari ameitumikia klabu hiyo kwenye michezo minne ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.

Makala Nyingine

More in Azam FC