Connect with us

Makala Nyingine

KUELEKEA UFUNGUZI AFL 2023, VIGOGO CAF WATEMBELEA KITUO TFF

Raisi wa TFF, Wallace Karia leo aliambatana na viongozi wa CAF ukanda huu kutoka Kigali, Rwanda sambamba na Makamu Mwenyekitiwa tatu wa CAF Ndugu Souleiman Waberi kutembelea Kituo ca Ufundi cha TFF kilichopo Kigamboni kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika kituo hicho.

Kwakuwa viongozi wetu wa juu, Raisi Infantino wa FIFA na Dr. Motsepe wa CAF watakuwa hapa kesho, viongozi wa ukanda huu ambao ofisi ipo Kigali na ndipo sisi tunawajibika napo wameona waje waangalie maandalizi na kama kila kitu kinaenda sawa ikiwemo kuangalia wapi patawekwa jiwe la msingi ukizingatia kituo hiki kitawekwa jiwe la msingi na Infantino, Motsepe na Mheshimiwa Waziri, Dr. Damas Ndumbaro. Kwahiyo ni utaratibu wa kawaida tu.

Aidha Makamu wa Raisi wa tatu wa CAF Ndugu Waberi naye alitoa neno la kuonyesha kuridhishwa na alichokiona.

Nimeridhishwa na kufurahishwa sana nanilichokiona kwenye kituo hiki. Kaka yangu Wallace Karia kafanya kazi kubwa sana hapa na anastahili pongezi. Kila kitu kipo sawa hapa na hata mipango aliyoieleza inaeleweka na inatia moyo hasa kwa soka la vijana, miaka 17, 15. Kazi nzuri sana.

Alisema Souleiman Waberi ambaye pia ni Raisi wa Shirikisho la soka la Djibout.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine