International Football

ROBERTINHO ANA IMANI NA WACHEZAJI WAKE KUELEKEA MCHEZO WA KESHO

Published on

Kocha wa klabu ya Simba Mbrazili Roberto Oliveira maarufu Robertinho amesema kuwa ana imani kubwa sana na uwezo na ubora wa wachezaji wake kuelekea mchezo wa kesho wa ufunguzi wa African Football League 2023 dhidi ya Al Ahly licha ya kuheshimu ubora wa wapinzani wake hao.

Tunawaheshimu wapinzani wetu ni moja ya timu kubwa Afrika lakini naamini kwenye uwezo wa wachezaji wangu na wote wapo vizuri. Naamini kesho tutacheza vizuri na tutashinda.

Robertinho alisema maneno hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo hii akizungumzia timu yake namna alivyoiandaa na utayari wa wachezaji wake wakekuelekea mchezo huo.

Aidha, Nahodha John Raphael Bocco naye alizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake huku yeye akisisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa hamasa.

Utakuwa mchezo mkubwa kwetu Simba na Tanzania kwa ujumla, tunategemea kuonyesha ubora wetu ili kupata matokeo mazuri na bahati nzuri tunacheza kwenye uwanja wa nyumbani.

Tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi ili kutushangilia na kutupa nguvu mwanzo mwisho.

Alisema Bocco.

Simba wanacheza mchezo wao wa kwanza wa michuano hii ya kwanza kufanyika barani Afrika kwenye uwanja wao wa nyumbani Benjamin Mkapa na kisha marejeano nchini Misri na mshindi wa jumla atavuka kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hii.

Popular Posts

Exit mobile version