Connect with us

CAF Champions League

AFL ITAHUSISHA TIMU 24 MSIMU UJAO.

Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika amesema msimu ujao African Football league itahusisha timu 24.

Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika Patrice Motsepe katika mkutano wake na wanahabari hii leo kuelekea ufunguzi wa michuano mikubwa Barani Africa ya African Football League kati ya Simba na Al ahly amesema, wanajivunia na mafanikio ambayo timu ya Taifa ya Morocco iliyapata kwenye fainali za kombe la Dunia nchini Qatar.

Tunatakiwa kuufanya mpira wa Afrika uvutie na ili uvutie ni lazima tushinde. Tunajivunia na kile walichokifanya Morocco, kufika nusu fainali katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika Qatar. Naamini kombe la Dunia lijalo tutafanya vizuri zaidi ya hapo walipoishia. Najivunia Tanzania, najivunia nchi zote 54 za Afrika, ninachotaka ni kuacha msingi wa soka kwaajili ya wengine.

Patrice Motsepe Rais wa CAF.

Motsepe amesema mikakati ya shirikisho la soka Barani Afrika ni kuhakikisha kombe la Dunia linakuja BArani Afrika na ili kombe liweze kuja Afrika lazima uwekezaji ufanyike hasa kwa vijana wa kike na wakiume wenye umri mdogo.

Tunataka kombe la Dunia lije Afrika lakini lazima tuanze na uwekezaji, kuendeleza mpira kwa wanaume na wanawake katika umri mdogo.

Patrice Motsepe amesema.

Motsepe amesema msimu ujao mashindano haya ya African Football Leagueyatahusisha timu takribani 24, na lengo ni kuonyesha vipaji vingi kutoka Afrika na mwisho wa siku wachezaji wapate pesa nyingi kutoka kwenye mpira wanaoutumikia.

Msimu ujao Ligi hii itahusisha timu 24, African Football League itaonyesha vipaji vingi sana, tunataka wapewe pesa nyingi kupitia mpira. Tunataka soka la Afrika liwalipe zaidi wachezaji wao kutokana na kile wanachokipata na kuhakikisha wanacheza mpira mzuri ili pia uwavutie wengi Duniani kuutazama mpira wetu.

Patrice Motsepe aliongeza.

Patrice Motsepe amesema kwasasa kuna ushirikiano wa kutosha kati ya shirikisho la soka la Afrika na shirikisho la soka Duniani (FIFA) na kwasasa kuna utaratibu wa FIFA kutoa mafunzo kwa marefa kutoka Afrika.

Namshukuru Rais wa FIFA Gianni Infatino ambaye kwasasa tumetengeneza uhusiano wa kuwapa elimu marefa wetu, kesho ya soka letu haitakuwa hivi tena. Tunataka zile pesa ambazo timu hizi zitapata zikawalipe wachezaji wazuri wa hizi klabu pamoja na wafanya kazi wake. Wameniambia Tanzania kuna timu mbili Simba na Yanga, nina zipenda zote hizi kwasababu hilo ndio jukumu langu.

Patrice Motsepe akizungumza na waandishi wa habari hii leo.

Mchezo wa ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly utapigwa leo Ijumaa October 20, saa 12:00 Jioni katika Dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League