Connect with us

International Football

KOMBE LA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE LAZINDULIWA, TANZANIA YASIFIWA

Raisi wa Shirikisho la Soka la Afrika, Dr. Patrice Motsepe, amezindua Kombe rasmi la AFRICAN FOOTBALL LEAGUE 2023 mchana huu kwenye hoteli ya kimataifa ya Hyatt mbele ya waandishi wa habari wakati pia akizungumzia mambo mbalimbali yahusuyo soka la Afrika sambamba na michuano hii mipya inayoanza leo.

Akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari, Motsepe alisema kuwa dhima kuu ya michuano hii ni kutumia fedha zitakazopatikana kuboresha michuano mingine chini ya CAF ikiwemo ya timu za taifa.

Tunatazamia sana kuboresha miundombinu ya soka la Afrika kwa wanachama wote 54 na kupitia mapato ya michuano hii tunaenda kuboresha mashindano yote chini ya CAF ikiwemo ya AFCON ya timu ya taifa zote.

Nimeulizwa hapa kama michuano hii itaua mashindano mengine ya shirikisho, nami niwatoe hofu kwani badala yake michuano hii itaenda kuipa uhai zaidi michuano yetu mingine kwa ukubwa zaidi.

Katika upande mwingine, Rais Motsepe aliimwagia sifa Tanzania kwa maandalizi mazuri mpaka hivi sasa

Nilipotoka nikapitia Dodoma na kuzungumza na Mheshimiwa Raisi wa Tanzania, tukatumia zaidi ya nusu saa kuongea kwakuwa tulikuwa tunajadiliana mambo mengi sio tu kuhusu AFL ila maandalizi ya AFCON 2027 hapa Tanzania. Aliniahidi kushughulikia mambo mengi kuhusiana na miundombinu, hospitali, hoteli, na zaidi viwanja. Niseme tu pongezi sana kwa serikali ya Tanzania na tutashirikiana nao ili kufanya AFCON ya kihistoria.

Alisema Motsepe akijibu swali kuhusu uboreshwaji wa Viwanja Tanzania kuelekea AFCON 2027.

Makala Nyingine

More in International Football