

Simba Sports Club, leo inakwenda kuandika historia kubwa sana kwa klabu na taifa kwa ujumla. Mbele ya viongozi wakubwa wa soka Barani Afrika na Duniani anakwenda kufungua mashindano makubwa barani Afrika dhidi ya mpinzani ambaye ni namba 1 kwa ubora na ukubwa Afrika, Al Ahly. Siku kubwa hii kwa soka la Tanzania.
Hata ukirudi mpaka mwaka 1985, itakuonyesha kuwa wawili hawa hakuna mbabe wa mwenzake kwenye michuano ya Afrika waliyokutana. Kati ya michezo 6 iliyowakutanisha, kila mtu kashinda mechi 3 na kila mtu kashinda kwake. Hakuna sare kati yao. Michezo minne waliocheza hivi karibuni inadhihirisha, 2019, Al Ahly akishinda 5-0 kwake na Simba akishinda 1-0 kwa Mkapa. Msimu wa 2021, kila mmoja akishinda 1-0 kwake.
Lakini hebu tuuzungumzie mchezo wenyewe wa leo, na Simba aingiaje kwenye mchezo huu ili apate matokeo, kitakwimu na kitaalamu.
MATOKEO YA MWISHO
Simba walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida FG kwenye mchezo wa ligi kuu magoli yakifungwa na Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri huku Al Ahly alishinda 3-1 dhidi ya Ismaily kwenye ligi kuu nchini Misri, magoli mawili ya Percy Tau na moja la Hussein El Shahat. Kwa matokeo haya ya mwisho yanaonyesha safu zote za ulinzi zinaruhusu magoli hivyo magoli yatapatikana mchezo wa leo kwa timu itakayofanya makosa mengi, itafungwa zaidi kwakuwa pia magoli ya kufunga yanapatikana.
MIFUMO:
SIMBA :4-2-3-1; Umekuwa ni mfumo mama wa Simba siku zote. Viungo wakabaji wawili wa kuwalinda mabeki lakini kutoa muunganiko kwa safu ya ushambuliaji kuanzia viungo watatu washambuliaji kwenda kwa mshambuliaji pekee. Ni mfumo unaokupa uwiano mzuri dhidi ya mpinzani kwa kuwa na viungo watano wanaokupa ukabaji ukiwa hauna mpira na ushambuliaji ukiwa na mpira. Ni rahisi pia kuruhusu mashambulizi kama viungo wa chini wakipotea lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa kutengeneza magoli.
AL AHLY : 4-3-3; Ni mfumo wanaoutumia sana Al Ahly pia kwenye mechi zao na hasa dhidi ya wapinzani ambao wana viungo wengi pia. Wakitumia kasi ya Percy Tau na Ufundi wa Hussein El Shahat pembeni kummlisha mshambuliaji wa kati aidha Anthony Modeste au Mahmoud Kahraba. Lakini Kiungo pia kina ugumu wa Aliou Dieng na Koka na Unyumbufu wa Emam Ashour. Al Ahly huwa hatari sana kwenye mfumo huu.
SIMBA IINGIE NA MFUMO GANI?
4-2-3-1 ili kuendelea kuwa na idadi kubwa ya viungo lakini itakuwa sawa zaidi kama kwenye viungo watatu wa juu akawepo Mzamiru Yassin kama Box to Box huku chini akicheza Sadio Kanoute na Fabrice Ngoma. Hii itawasaidia kufanya ukabaji wa mtu na mtu kwenye kiungo na kuwapa asafu ya ushambuliaji nafasi ya kucheza. Kucheza hivi kutamaanisha viungo watatu wa Al Ahly wote watakuwa wanakabwa na Mzamiru, Kanoute na Ngoma kukata mawasiliano. Itakuwa ni 4-2-3-1 yenye kivuli cha 4-3-3 Shambulizi(Attack).
WA KUCHUNGWA
AL AHLY : Percy Tau amekuwa na nyakati nzuri hivi karibuni na mwalimu Koller amekuwa akimmtumia kama msaidizi wa mshambuliaji akitokea pembeni kama ilivyo kwa Hussein El Shahat na wote hawa wana uwezo pia wa kuingia ndani na kufunga au kutengeneza nafasi kwa mshambuliaji wa kati. Wanapaswa kuangaliwa sana hawa.
REKODI MPYA?
SIMBA: Hawajawa na nyakati nzuri kwenye hatua za mtoano hasa Robo fainali kama hivi, wanakutana na Al Ahly ambayo huwa bora zaidi kwenye hatua hizi, je wataweka rekodi mpya kwa kufuzu Nusu fainali na kuiondosha Al Ahly kwenye hatua ya mtoano?
AL AHLY : Mabingwa wa takribani kila kombe chini ya CAF upande wa vilabu. Mabingwa mara 11 wa CAF Champions League na Klabu yenye makombe mengi zaidi Afrika, je itaenda kutwaa kombe jingine jipya chini ya CAF? Watakivuka kihunzi cha Simba?
Tukutane kwa Lupaso.

Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 1 year agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 1 year agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 12 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 12 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 1 year agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...