Connect with us

African Football League

SIMBA YAIANZA SAFARI KUELEKEA MISRI.

Klabu ya Simba imeianza safari hii leo kuelekea nchini Misri katika mchezo wa marejeano ya African Football League dhidi ya Al Ahly.

Klabu ya Simba imeanza safari hii leo kuelekea nchini Misri kupitia Addis Ababa nchini Ethiopia kwaajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Al Ahly wa michuano ya African Football League, mchezo ambao utapigwa katika dimba la Cairo, Jumanne, October 24. Simba itafika na kupumzika Addis Ababa kabla ya kuanza safari ya kuunganisha kuelekea nchini Misri majira ya saa nne usiku na inatarajia kufika nchini Misri saa sita au saa saba usiku.

Kwa mujibu wa Ofisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema sababu za timu hiyo kusafiri mapema ni kuwapa nafasi wachezaji kuzoea mazingira, kupata muda wa kupumzika na muda wa kufanya mazoezi lakini pia kupata maandalizi ya kutosha nje ya uwanja.

Mshambuliaji wa klabu ya Al Ahly Percy Tau akichuana na mlinzi wa Simba Mohamed Hussein katika mchezo wa ufunguzi wa African Football League katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

Kabla ya kuondoka nchini Ofisa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally amewataka wana Simba wasiwe na wasiwasi kwani timu yao imefanya maandalizi ya kutosha na Al Ahly sio timu ya kuisumbua Simba huku akitoa tahadhari kuwa Al Ahly inaweza kushinda lakini sio kwa kiwango cha kuidhalilisha klabu ya Simba.

Utawala wa Al Ahly mbele ya Simba uliisha 2018, 2019 wakati anaifunga simba goli tano (5), baada ya hapo utawala wao ndani ya Simba ukaisha kabisa, sasa tukabaki tunalingana, ukiangalia mechi yetu na wao baada ya ile ya goli tano, tulicheza mechi mbili (2) na zote ametufunga goli moja (1) kwa tabu kwelikweli, sasa hiyo ni Simba ya 2019/2020, sasa hii ni Simba ya 2022/23 lazima uone kuna maendeleo makubwa kwenye Simba yetu.

Ahmed Ally akizungumza na wanahabari kabla ya kuanza safari.

Mchezo wa kwanza wa Simba na Al Ahly uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam ulimalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2. Ili Simba iweze kufuzu kuelekea hatua ya fainali inatakiwa ipate ushindi wa aina yoyote ama itoe sare ya kufungana magoli 3-3 na kuendelea, kama watatoa sare ya 2-2 au 1-1 au 0-0 Al Ahly atafuzu kwenda hatua inayofuata.

Makala Nyingine

More in African Football League