Connect with us

African Football League

TP MAZEMBE KUKIPIGA NA ESPERANCE UWANJA WA MKAPA LEO.

TP Mazembe imechagua kucheza mchezo wake dhidi ya Esperance leo uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na uwanja wake kutokukidhi matakwa ya CAF.

Klabu ya TP Mazembe itashuka dimbani hii leo ikiwa nyumbani kuwaalika Esperance de Tunis kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainal wa michuano mipya Barani Afrika ya African Football League. TP Mazembe wamechagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa nchini Tanzania kutokana na dimba lake kukosa sifa za kuchezewa mchezo huu.

18:00 TP Mazembe [DR Congo] vs Esperance de Tunis [Tunisia]

Uwanja: Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

TP Mazembe katika michezo kumi (10) ya mwisho kwenye michuano yote, imeshinda michezo saba (7), na kutoa sare mchezo mmoja (1) na imepoteza michezo miwili (2). Katika michezo mitano (5) ya mwisho ya kimataifa, imeshinda michezo miwili (2), na imepoteza michezo mitatu (3).

Esperance de Tunis katika michezo kumi (10) ya mwisho kwenye michuano yote, imeshinda michezo mitano (5), imetoa sare michezo minne (4), imepoteza mchezo mmoja (1). Katika michezo mitano (5) ya mwisho ya kimataifa, imeshinda mchezo mmoja (1), imepoteza mchezo mmoja (1), imetoa sare tatu (3).

Timu hizi zimekutana mara kumi (10) kwenye michuano ya kimataifa, TP Mazembe imeshinda michezo mitatu (3), michezo hiyo imeshinda ikiwa nyumbani. Esperance imeshinda michezo minne (4) yote imeshinda ikiwa nyumbani. Timu hizi zimetoka sare mara mbili (2) kila timu ikitoa sare katika diMba la mwenzake.

Kipigo kikubwa ambacho Esperance aliwahi kukutana nacho kutoka kwa TP Mazembe ni cha goli 5-0 Lubumbashi.

Leo wanakutana kwa mara ya kwanza katika michuano hii ya African Football League katika dimba la Benjamin Mkapa, Tanzania. TP Mazembe ndiye mwenyeji wa mchezo huu.

Matokeo ya michezo mingine ya African Football League ni:

Simba [Tanzania] 2-2 Al Ahly [Misri].

Petro Atletico [Angola] 0-2 Mamelodi Sundowns [South Africa].

Makala Nyingine

More in African Football League