Connect with us

Michezo Mingine

PAZI YATINGA ELITE 16 ROAD TO BAL 2024, KIBABE.

Klabu ya Mchezo wa mpira wa kikapu ya Pazi imefanikiwa kuwa miongoni mwa timu 16 zitakazochuana kwenye raundi ya pili (ELITE I6)  ya kutafuta timu 6 za kwenda kushiriki michuano ya Mpira wa Kikapu ya Afrika yani BAL(Basketball Africa League) 2024 wakiipeperusha Bendera ya Tanzania.

Pazi ilifanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ya Kundi C kwenye raundi ya kwanza ya kufuzu kuelekea raundi ya pili na kuongoza kundi.

ROAD TO BAL: 2024, inakuwa ni toleo la nne tangu kuanzishwa michuano hii mwaka 2019. Timu shiriki huwa ni mabingwa wa Nchi wanachama wa shirikisho la Mpira wa Kikapu, FIBA Africa wa michuano ya ligi za nchi za msimu uliomalizika. PAZI ni bingwa wa Tanzania msimu wa 2023.

Timu hugawanywa kwenye West Division na East Division na kisha makundi A-E kupata timu 6(5 vinara wa makundi na 1 mwenyeji), kundi A limetoa timu 2 kwakuwa timu za Elan Coton na Nigelec zilijitoa mashindanoni hivyo kufanya Timu 7 kufuzu kutoka kwenye raundi ya 1 kujiunga na timu sita(6) bora kutoka kwenye msimu uliopita wa mashindano ya Elite 16, yani timu 3 bora kutoka kwenye divisheni mbili za kimashindano.

Timu hizi 13 zinaongezewa timu 2 za kuchaguliwa kama “Wild Card” na timu nyingine huwa ni NBA Academy ya nchini Ghana. Kufanya jumla ya timu 16 zitakazochuana kupata timu 6 za kwenda kushiriki BAL 2024, 3 Kutoka kila Divisheni.

TIMU ZILIZOFUZU NI KAMA IFUATAVYO:

WEST DIVISION(DIVISHENI YA MAGHARIBI)

KITUO: ABIDJAN, IVORY COAST

1. AL AHLY BENGHAZI – LIBYA

2. FUS RABAT – MOROCCO

3. BANGUI SPORTING – JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

4. FAP – CAMEROON

5. FERROVIARIO DA BEIRA – MOZAMBIQUE(WASHINDI WA PILI WA DIVISHENI 2023)

6. CAPE TOWN TIGERS – AFRIKA YA KUSINI(MABINGWA WA DIVISHENI 2023)

7. CITY OILERS – UGANDA(WASHINDI WA TATU WA DIVISHENI 2023)

8. NBA ACADEMY – GHANA

EAST DIVISION(DIVISHENI YA MASHARIKI)

KITUO: JOHANNESBURG, AFRIKA YA KUSINI

1. PAZI –TANZANIA

2. DOLPHINS – BOTSWANA

3. COSPN – MADAGASCAR

4. ABC FIGHTERS – IVORY COAST (MABINGWA WA DIVISHENI 2023)

5. SLAC – GUINEA(WASHINDI WA PILI WA DIVISHENI 2023)

6. STADE MALIEN – MALI

7. WILD CARD

8. WILD CARD

Ratiba kutoka hivi karibuni na utaipata hapa hapa.

Makala Nyingine

More in Michezo Mingine