Connect with us

African Football League

SIMBA INA WAKATI MGUMU KWA AL AHLY.

Magori amesema klabu hiyo ina wakati mgumu kuelekea mchezo wa marejeano dhidi ya Al Ahly nchini Misri.

Mtendaji mkuu wa zamani wa klabu ya Simba ambaye kwasasa ni mshauri wa Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji, Crescentius Magori, kupitia kipindi cha Sports Extra kinachorushwa na Clouds fm radio amesema klabu ya Simba ina wakati mgumu kwenye mchezo wa marejeano dhidi ya Al Ahly na hautakuwa mchezo rahisi.

“Simba tuna wakati mgumu sana katika mchezo na Al Ahly wa marudio na wala Tusijidanganye, inabidi wachezaji wakafanye kazi zaidi na kujitolea, ingawa hakuna kinachoshindikana kwani mwaka 2003 tuliwatoa mabingwa Zamaleki enzi hizo huko huko kwao kipindi ambacho wengi hapa Tanzania walikua wametukatia tamaa”.

Mshauri wa Rais wa heshima wa klabu ya simba, Crescentius Magori.

Aidha hadi hivi sasa bado kuna sintofahamu kuhusiana na goli la ugenini kama lina hesabika kwenye mashindano haya ama limefutwa.

Kanuni za mashindano ya AFL zinaelekeza kuwa goli la ugenini linafanya kazi katika mashindano haya.

Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana goli 2-2 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam. Simba inalazimika kupata ushindi ama sare ya 3-3 ili isonge mbele kwenye michuano hii kama mchezo ukimalizika kwa sare ya 2-2 changamoto ya mikwaju ya penati itafuata.

Makala Nyingine

More in African Football League