Connect with us

AFL

SIMBA KUYACHOTA MABILIONI YA AFL MISRI?

Wawakilishi pekee kutoka nchini Tanzania Simba SC leo itakuwa ugenini kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly baada ya mchezo wa awali kuchezwa nchini Tanzania na kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Endapo Simba SC itafanikiwa kupata matokeo mazuri yatakayowavusha kuingia nusu fainali ya mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo,Misri leo kuanzia saa 11 joni, itawahakikishia kiasi cha Dola 1.7 milioni sawa na Tsh4.2 bilioni, kutoka kwa waandaji wa mashindano hayo mapya kabisa barani Afrika.

Ingawa Simba imekuwa haina historia nzuri kwa mechi ambazo imekuwa ikicheza nchini Misri kwani haijawahi kupata ushindi wa ndani ya dakika 90 hata mara moja.

Katika mechi 10 za mashindano tofauti ambazo Simba imecheza nchini Misri, imefungwa michezo tisa na imetoka sare mara moja tu huku ikifunga mabao mawili huku ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 21.

Dhidi ya Al Ahly, Simba imekutana nao mara tatu katika mashindano ya kimataifa ambapo imepoteza zote pasipo kufunga bao hata moja huku ikifungwa mabao nane.

Katika hatua nyingine mchezo wa leo utachezeshwa na refa Jean Jacques Ndala kutoka DR Congo ambaye atasaidiwa na Jerson dos Santos wa Angola na Arsenio Marengula wa Msumbiji huku refa wa akiba akiwa ni Messie Nkounkou wa Congo.

Refa Ndala amekuwa na historia nzuri na Simba ambapo katika mechi tatu alizochezesha, klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi mara mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Galaxy 0-2 Simba SC
Simba 1-0 RS Berkane
JS Saoura 2-0 Simba

Makala Nyingine

More in AFL