Connect with us

Manchester United

ERIKSEN NI BORA KULIKO AMRABAT.

Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes amesema mchezo wa Manchester United dhidi ya Copenhagen ulikuwa kama wa Europa.

Nyota wa zamani wa kikosi cha Manchester United Paul Scholes amemwambia kocha wa kikosi cha Manchester United Eric Ten Hag, kuwa Christian Eriksen ni bora kuliko Sofyan Amrabat ambaye bado anapambana kuonyesha uwezo wake tangu asajiliwe kwa mkopo kutoka Fiorentina.

Eriksen aliingia kipindi cha pili katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Barani Ulaya wakati Manchester United ikiibuka na ushindi wa goli 1-0 nyumbani dhidi ya Copenhagen Jana. Manchester United walikuwa wanahangaika kutengeneza nafasi na kuingia kwa Eriksen kuliongeza ubunifu kwenye eneo la mwisho.

Paul Scholes amemwambia Eric Ten Hag kuwa anapaswa kumuanzisha kwenye kikosi cha kwanza kuliko kuanza na Amrabat ambaye bado anahangaika kuingia kwenye mfumo.

Ni kama tulikuwa tunaangalia Ligi ya Europa kwenye kipindi cha kwanza, ni kama mpira wa Alhamis tu, mpira mbovu. Kipindi cha pili ilikuwa vizuri angalau baada ya kuingiza wachezaji wazuri. Kumuingiza Eriksen mchezaji mzuri sana, bila kumkosea heshima Amrabat, ni mzuiaji mzuri lazima atafanya hivyo tu, lakini hawezi kuanzisha mashambulizi, lakini Eriksen anaweza. Uliona mikimbio aliyoifanya, ghafla Bruno na Garnacho nao wakaingia kwenye mchezo, kwa dakika 10-20 ilionekana kama timu tena.

Paul Scholes akizungumza kupitia TNT Sports

Eriksen msimu huu amekuwa akianzia benchi katika kikosi cha Manchester United, ameanza michezo minne (4) pekee katika michezo kumi na moja (11) ambayo timu hiyo imecheza katika mashindano yote. Scholes anaamini Eriksen anaweza kuisaidia timu pindi inapokutana na timu inayojilinda.

Christian muda wote anawaza kushambulia. Aliuleta mpira ambao hatukuwa naokipindi cha kwanza – Copenhagen walikuwa vizuri sana hadi uwafungue, Christian Eriksen alikuwa anapiga pasi sahihi.

Paul Scholes aliongeza.

Makala Nyingine

More in Manchester United