Connect with us

NBC Premier League

LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA LEO.

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inataraji kuendelea hii leo kwa michezo mitatu kufanyika katika viwanja vitatu tofauti nchini, hizi ni takwimu za michezo yote mitatu.

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja vitatu tofauti tofauti nchini.

14:00 JKT TANZANIA vs TABORA UNITED.

UWANJA: Uhuru Stadium, Dar Es Salaam

  • JKT Tanzania na Tabora United hazijawahi kukutana kwenye Ligi kuu Tanzania Bara leo itakuwa ni kwa mara ya kwanza kukutana. Timu hizi mbili zilikuwa Ligi daraja la kwanza msimu uliopita, JKT Tanzania alimaliza kinara mbele ya Tabora United kwenye msimamo wa Ligi.
  • Timu hizi zimekutana mara nne (4) Kwenye Championship, JKT Tanzania akishinda mara mbili (2), Tabora United ikishinda mara mbili (2).
  • JKT Tanzania imecheza michezo sita ya Ligi kuu Kandanda Tanzania Bara msimu huu, imeshinda michezo miwili (2), imepoteza michezo miwili (2) na imetoa sare michezo miwili (2), Inashika nafasi ya saba (7) ikiwa na alama nane (8).
  • Tabora united imecheza michezo sita (6) ya Ligi kuu msimu huu, imeshinda michezo miwili (2), imepoteza mchezo mmoja (1) na imetoa sare michezo mitatu (3) ipo nafasi ya tano (5) ya Msimamo wa Ligi ikiwa na alama tisa (9).

16:00 COASTAL UNION vs MASHUJAA FC

UWANJA: CCM Mkwakwani, Tanga

  • Hii itakuwa mara ya kwanza kwa klabu hizi mbili kukutana katika michezo ya Ligi kuu Kandanda Tanzania Bara, hazina historia yoyote ya kukutana.
  • Coastal Union ni timu kongwe kwenye Ligi ukilinganisha na Mashujaa (Kigoma), imecheza michezo sita (6), haijaonja ladha yoyote ya ushindi msimu huu chini ya kocha wake Mwinyi Zahera, imetoka sare michezo mitatu (3), imepoteza michezo mitatu (3), ina alama tatu (3) na ipo nafasi ya 15 ya msimamo wa Ligi Kuu.
  • Mashujaa hadi hivi sasa licha ya ugeni wao kwenye Ligi wamecheza michezo mitano (5), wameshinda michezo miwili (2), wamepoteza mchezo mmoja (1) na wametoa sare michezo miwili (2), wapo nafasi ya sita (6) ya msimamo wa Ligi wakiwa na alama nane (8).

21:00 DODOMA JIJI FC vs KAGERA SUGAR

UWANJA: CCM Jamhuri, Dodoma.

  • Kagera Sugar imepoteza michezo miwili (2), imeshinda michezo miwili (2), na kutoa sare michezo miwili (2) imekusanya alama nane (8) katika nafasi ya nane (8) ya msimamo ikiwa imecheza michezo sita (6).
  • Dodoma Jiji imecheza michezo sita hadi hivi sasa, ikishinda mchezo mmoja (1), imetoa sare michezo mitatu (3), imepoteza mchezo mmoja (1), ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama sita (6).
  • Timu hizi zimekutana mara sita (6), Dodoma Jiji ikishinda mara moja (1), Kagera Sugar ikishinda mara moja (1), na zimetoka sare mara nne (4).
  • Katika michezo ambayo klabu hizi zimekutana jumla ya magoli saba (7) yamefungwa, Dodoma ikifunga magoli manne (4), na Kagera ikifunga magoli matatu (3).

Makala Nyingine

More in NBC Premier League