Ligi ya mabingwa Barani Ulaya inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo nane (8) kupigwa.
19:45 BARCELONA vs SHAKHTAR DONETSK
UWANJA: Camp Nou
- Mchezo huu unaweza kufuatiliwa na Watanzania wengi kutokana na nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania Novatus Dismas ambaye anakipiga kwenye klabu ya Shakhtar Donetsk.
- Novatus ni miongoni mwa nyota waliosafiri na kikosi hadi nchini Hispania kwaajili ya mchezo huo.
- Kocha aliyepita alikuwa akimpa nafasi zaidi ya kucheza Novatus Dismas kwenye kikosi chake, jambo ambalo wanalisubiri watanzania wengi ni kuona kama kocha huyu mpya atatoa nafasi zaidi kwa Nova ama lah.
- Klabu ya Barcelona inaingia katika mchezo huu ikiwa na majeruhi saba (7) wa kikosi cha kwanza, hii inamfanya kocha wa kikosi hicho Xavi kutumia vijana zaidi katika michezo ya hivi karibuni. Leo pia inatazamiwa kuwa huenda akawatumia vijana kutoka kwenye Academy ya kikosi hicho.
- Shakhtar Donetsk inaingia katika mchezo huu hii leo ikiwa imetoka kumtambulisha kocha wake mpya Marino Pušić jana baada ya Patrick van Leeuwen kuachia ngazi. Huu utakuwa mchezo wake wa kwanza akiwa anaiongoza klabu hiyo ambayo amejiunga nayo jana. Marino amewahi kuzinoa klabu za Feyenood na FC Twente.
Kocha msaidizi wa kikosi cha Shakhtar Donetsk Darijo Srna amesema walikuwa wakiwasiliana na kocha mkuu kwa muda mrefu na leo anaweza kuwa kwenye benchi la ufundi la Shakhtar.
Nimekuwa nikiwasiliana na kocha wetu mpya kwa muda mrefu. Tumezungumza kuhusiana na mchezo wa leo. Kocha mkuu atakuwa kwenye benchi hii hii leo sambamba na mimi na kocha mwingine msaidizi.
Darijo Srna, Kocha msaidizi Shakhtar Donetsk.
kwa upande wa nyota wa kikosi hicho Georgiy Sudakov amesema kila mchezaji alikuwa na furaha ya kumkaribisha kocha mpya ndani ya kikosi chao. Sudakov ameleza maandalizi yao kuelekea mchezo wa leo.
Tupo tayari kwa asilimia 100 kwaajili ya mchezo, tunaelewa nini Barcelona wanataka na kipi wanataka kuionyesha Dunia, lakini tuna wachezaji wazuri wenye uwezo, hivyo tunachotakiwa ni kujiamini.
Georgiy Sudakov, kiungo wa Shakhtar.
Kwa upande wa kocha wa kikosi cha Barcelona Xavi Hernandez amesema kuwa na majeruhi wengi kwenye kikosi chake sio kigezo cha kutokufanya vizuri japo ina waumiza kwa namna moja ama nyingine.
Kuhusu swa la majeruhi sio swala la kufikiria japo ndio hali tuliyonayo kwasasa. Hivyo ndivyo ilivyo na itabaki hivyo, baadhi ya wachezaji ni majeruhi, Gavi ana adhabu… lakini hatupo hapa kulaumu lakini kucheza vizuri zaidi ya kipindi cha kwanza cha siku ile. Kuhusu kuwa na majeruhi wengi sio tatizo.
Xavi Hernandez
Kwa upande wa Ferran Torres mshambuliaji wa kikosi hicho amesema wachezaji wamejiandaa vyema kuhakikisha wanaipatia ushindi timu yao.
Nimejiandaa vyema na majukumu yangu kwenye eneo la ushambuliaji. Najihisi kama mzee sasa [kulinganisha na wachezaji wengi vijana ndani ya kikosi cha Barcelona]. Najitahidi kuwapa ushauri hawa wachezaji ambao wana nguvu na wanaojitambulisha kwenye kikosicha kwanza. Wana hofu sana, lakini wanapaswa kuikabili, wana thamani kubwa sana.
Ferran Torres mshambuliaji wa Barcelona.
MICHEZO MINGINE ITAKAYOPIGWA HII LEO.
19:45 FEYENOOD vs LAZIO
22:00 CELTIC vs ATLETICO MADRID.
22:00 NEWCASTLE UNITED vs BORUSSIA DORTMUND
22:00 PSG vs AC MILAN
22:00 RB LEIPZING vs FK CRVENA ZVEZDA
22:00 YOUNG BOYS vs MANCHESTER CITY
22:00 ROYAL ANTWERP vs FC PORTO