Connect with us

Al-Nassr

RONALDO KUMSUBIRI DE BRUYNE AL NASRI

Klabu ya Al-Nasr ya Saudi Arabia tayari inafikiria jinsi ya kuimarisha kikosi chao katika kipindi hiki cha majira ya baridi kali. Hasa, mabosi wa klabu hiyo wanatarajia kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji na klabu ya Manchester City Kevin De Bruyne.

Taarifa zinasema, tayari klabu ya Al-Nasr kutoka nchini Saudi Arabia imefanya mazungumzo na wakala wa kiungo huyo wa Ubelgiji ili kupanga mkutano wa majadialino na kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo katika siku za karibuni.

Al-Nasr kujaribu kumshawishi De Bruyne kuhamia kwao litakuwa jambo sahihi. Wanataka kumwambia mchezaji kuhusu kuvutia kwa mkakati wao wa muda mrefu. Ni jambo la busara kukiri hadharani kwamba ni kweli De Bruyne yuko na mkataba halali na klabu yake ya Manchester City hadi 2025.

Alisema De Koster ambaye ni wakala wa mchezaji wa Manchester City Kevin De Bruyne

Mpaka sasa Kevin De Bruyne amecheza mechi mbili pekee msimu huu kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara, hivyo mazungumzo kuhusu mkataba mpya yamesitishwa hadi atakapopona kabisa. Ikiwa uhamisho huo utafanikiwa kukamilika, De Bruyne atakuwa mmoja wa wanasoka mashuhuri ambao watakuwa wamehamia Mashariki ya Kati na kuungana na wapinzani wake wengi wa zamani aliowahi kucheza nao Ligi Kuu ya nchini Uingereza

Makala Nyingine

More in Al-Nassr