Connect with us

EPL

DAVID DE GEA KUREJEA MANCHESTER UNITED.

Klabu ya Manchester United imepanga kumsajili nyota wake wa zamani David De Gea katika dirisha dogo la mwezi January.

Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Manchester United David De Gea anatajwa kurejea ndani ya kikosi cha Manchester United kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January.

De Gea anatajwa kujiunga na kikosi hicho kutokana na kiwango alichokionyesha mlinda lango wa sasa Andre Onana tangu alipojiunga na kikosi hicho mapema dirisha kubwa lililopita. Lakini pia sababu nyingine inayotajwa Manchester United ifikirie kumsajili tena De Gea kwa mkataba wa muda mfupi ni kutokana na mwezi January Andre Onana kwenda kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON).

De Gea amekuwa akionekana na nyota kadhaa wa Manchester united mara kwa mara kitu ambacho kinaendelea kuwafanya mashabiki waamini kuwa anaweza kurejea mwezi January. De Gea amepost kwenye ukurasa wake wa X emoji ya kutafakari, mashabiki wengi wameielezea kama anafikiria kurejea tena klabuni hapo.

De Gea ameshinda Ligi kuu, FA, kombe la Ligi, na Europa wakati akiitumikia Manchester United. De Gea ndiye golikipa mwenye hati safi (Cleansheet) nyingi kuliko golikipa yoyote kwenye historia ya Manchester United, na ana tuzo nne za mchezaji bora wa msimu akiwa na kikosi cha Manchester United.

Makala Nyingine

More in EPL