Connect with us

NBC Premier League

MASHUJAA FC, HAITISHI UGENINI

Timu ya Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma inayoshiriki ligi kuu ya NBC bado haijaonesha maajabu ikicheza nje ya Uwanja wa Lake Tanganyika (uwanja wao wa nyumbani), imepoteza mechi mbili [2] mfululizo kati ya tatu [3] ambazo imecheza nje ya mkoa wa Kigoma.

Katika mechi tatu za kwanza ambazo Mtimu ya Mashujaa ilicheza nyumbani, ilifanikiwa kukusanya alama saba hiyo ni baada ya kushinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

Baada ya msimu huu kuanza, Mashujaa ilianzia nyumbani kwa mechi tatu mfululizo ambazo ilishinda mbili na kutoka sare moja. Baada ya hapo ikasafiri nje ya Kigoma kwa mechi tatu, ambapo imepoteza mechi mbili na kuambulia sare moja!

MATOKEO YA MASHUJAA LIGI KUU 2023|24
Mashujaa 2-0 Kagera Sugar
Mashujaa 0-0 Geita Gold
Mashujaa 2-0 Ihefu SC
Namungo 0-0 Mashujaa
JKT Tanzania 1-0 Mashujaa
Coastal Union 2-0 Mashujaa

Mashujaa ikiwa ugenini imeambulia alama moja tu baada ya sare dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliochezwa mkoani Lindi, Ruangwa katika uwanja wa Majaliwa, huku ikiwa imepoteza alama nane kati ya tisa za ugenini. Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC, Mashujaa FC itakuwa nyumbani kwa mechi tatu mfululizo.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League