Connect with us

NBC Premier League

HATUWAOGOPI SIMBA, TUNAWAHESHIMU – BASENA

Kocha wa timu ya Ihefu, Moses Basena, ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Simba msimu wa 2011 amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kuchuana na Simba kwenye mchezo wa kesho wa ligi kuu ya NBC na maeneo yote ya msingi tayari wamefanyia kazi kupambana na mpinzani mgumu na timu kubwa kama Simba.

Tunacheza dhidi ya timu kubwa sana. Wametoka kucheza michuano mipya mikubwa ya AFL, wamefuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa lakini ni timu ambayo bado haijafungwa kwenye ligi. Hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya na tunahitaji kuwa makini kwenye maeneo mengi ikiwemo kuwa na nidhamu kubwa ya mchezo, kuwaheshimu na kuziba mianya yote ya wao kucheza.

Aidha kwa upande wa wachezaji, Mlinda mlango wa timu hiyo, Hussein Masalanga alisema kuwa wanajua wanacheza na timu ya aina gani lakini na wao wamejipanga vizuri kupambana.

Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa wametoka kucheza kwenye mashindano makubwa Afrika. Nafikiri kila mchezo una namna ya kueendea, na walimu wetu watakuwa na mpango ambao sisi itakuwa ni jukumu letu kufuata ili tuweze kupata matokeo dhidi yao.

Ihefu SC watakutana na Simba kwa mara ya kwanza msimu huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 28, 2023 majira ya Saa 1:00 Usiku.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League