
Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini. Mchezo mkubwa unaotazamwa na wengi ni ule unaomhusisha Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo Young Africans dhidi ya Singida Foutain Gate kutoka mkoani Singida.

16:00 KMC vs TANZANIA PRISON
- Timu hizi zimekutana mara sita (6) tangu KMC ipande daraja msimu wa 2020/21.
- KMC imeshinda michezo miwili (2) pekee na ushindi mkubwa ulikuwa ni wa 2-0.
- Tanzania Prison imeshinda mara mbili (2) na ushindi mkubwa ulikuwa ni wa 2-1.
- Timu hizi zimetoka sare mara mbili (2) moja ya bila kufungana na nyingine ya goli 1-1.
- KMC imefunga magoli sita (6) na Tanzania Prison wamefunga magoli matano (5).
- KMC ipo nafasi ya nne (4) ya msimamo wa Ligi msimu huu ikiwa imekusanya alama 11, imeshinda michezo mitatu (3), imetoa sare michezo miwili (2), imepoteza mchezo mmoja (1) katika michezo sita (6) iliyocheza.
- Tanzania Prison ipo nafasi ya kumi na nne (14)ya msimamo wa Ligi msimu huu ikiwa imekusanya alama tano (5), imeshinda mchezo mmoja (1), imetoa sare michezo miwili (2), imepoteza michezo mitatu (3) katika michezo sita (6) iliyocheza.
18:15 YOUNG AFRICANS vs SINGIDA FOUNTAIN GATE
UWANJA: Benjamin Mkapa
- Singida Fountain Gate ilipanda daraja msimu wa 2022/23 na imekutana na Young Africans mara mbili (2) kwenye michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na imepoteza michezo yote.
- Tangu Singida ipande daraja haijawahi kuonja ushindi wowote mbele ya Young Africans, imewahi kupokea kipigo kizito cha goli 4-1 ikiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
- Mchezo huu utachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa hii leo.
- Katika michezo sita (6) ya Ligi kuu ambayo Young Africans imecheza hadi hivi sasa imeshinda michezo mitano (5), imepoteza mchezo mmoja (1), ina alama 15 ikiwa kinara wa Ligi hadi hivi sasa.
- Young Africans Imefunga magoli kumi na nane (18), imeruhusu magoli manne (4).
- Singida Fountain Gate imecheza michezo sita (6), imeshinda michezo miwili (2), imetoa sare michezo miwili (2), imepoteza michezo miwili (2), ina alama nane (8) katika nafasi ya tisa (9) ya msimamo wa Ligi.
- Singida Fountain Gate imefunga magoli sita (6), imefungwa magoli sita (6).

20:00 ZAM vs NAMUNGO
UWANJA: Azam Complex
- Timu hizi zimekutana mara tano (5) kwenye Ligi, Azam imeshinda mara nne (4) na Namungo imeshinda mara moja (1) na ikishuhudiwa sare moja (1).
- Namungo imefunga magoli matatu (3), Azam imeifunga Namungo magoli matano (5).
- Namungo imecheza michezo sita (6) ya Ligi kuu, haijapata ushindi wowote, imetoa sare michezo mitatu (3) na kupoteza michezo mitatu (3) ipo nafasi ya 16 ya msimamo wa Ligi.
- Namungo wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wametoka kuachana na kocha wake mkuu Cedric Kaze.
- Namungo imefunga magoli matatu (3) na imefungwa magoli saba (7).
- Azam FC imechez michezo sita (6) ya Ligi kuu, imeshinda michezo minne (4), imetoa sare mchezo mmoja (1) na imepoteza mchezo mmoja (1) ipo nafasi ya tatu (3) ya msimamo wa Ligi.
- Azam FC imefunga magoli 12 na imeruhusu magoli matano (5) kwenye Ligi hadi hivi sasa.
- Mchezo huu utapigwa Azam Complex.

Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 1 year agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 1 year agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 12 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 12 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 1 year agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...