KMC na Tanzania Prisons wametoka sare ya 1-1 ikiwa sare ya pili mfululizo kwa timu zote mbili kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, Dar es Salaam.
KMC waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya 8 ya mchezo,Waziri Junior Shentembo alipata nafasi na kuachia shuti lakini lilikuwa chamtoto mbele ya Yona Amos.
Hali ya unyevu uwanjani, na maji sehemu kadha za kiwanja, kulifanya kwa kiasi Fulani tukose burudani ya mchezo tuliyoitegemea lakini hata hivyo bado nafasi ziliendelea kutengenezwa kwa timu zote mbili. Dakika ya 26, Prisons walidhani wamepata penati baada ya kiungo wao mshambuliaji, Edwin Balua kufanyiwa madhambi kwenye eneo la goli la KMC na Freddy Tangalo, lakini muamuzi alikuwa na mawazo tofauti.
Dakika ya 30, Prison walilisakama lango la Prisons baada ya Edwin Balua kupiga shuti lililowababatiza mabeki baada ya mwendo mzuri kati yake na Zabona Mayombya. Hata hivyo kona haikuzaa matunda.
Dakika ya 35, KMC walijibu mashambulizi na safari hii Ibrahim Elias alipokea pasi nzuri kutoka kwa Awesu Awesu lakini alikuwa na mambo mengi na mpira wake kuokolewa na kuwa shambulizi la kujibu, Jeremiah Juma akipokea mpira na kusogea mbele kidogo kabla ya kuachia shuti kali lililopanguliwa na Wilbol Maseke kabla ya kwenda kuudaka tena.
Dakika ya 39 ya mchezo, Awesu alichezewa madhambi na Joshua Nyantini na Ibrahim Elias Mao alipiga vizuri mpira wa adhabu uliokuwa ukielekea langoni lakini Yona Amos alikuwa makini na kuutoa. Kona haikuwa na manufaa kwa KMC.
Mpaka dakika ya 45 ya mchezo bado milango ni migumu, lakini mashambulizi yalikuwa ya timu zote mbili kujaribu kutafuta goli kwa nyakati tofauti. Lakini mpaka tunakwenda mapumziko, 0-0.
Kipindi cha pili Wenyeji waliingia bila kufanya mabadiliko yoyote la wageni Prisons wao walifanya mabadiliko kwenye safu yao ya Ushambuliaji kwa Kumuingiza Messi Roland Atangana badala ya Mambote Batshie.
Dakika ya 53 ya mchezo, Wilbol Maseke alijifunga mwenyewe baada ya kuuzamisha kimiani mpira wa kona ulioonekana kama hauna madhara yoyote kutoka kwa Zabona Mayombya kwenye harakati za kutaka kuuhakikisha unakwenda nje, juu ya lango, akaugusa na mkono na kuelekeza nyavuni. 1-0
Mechi ikiwa imeanza kuchangamka, dakika ya 57, Edwin Balua alipokea pasi kutoka kwa Joshua Nyantini na kupiga krosi maridadi iliyomkuta Jeremiah Juma lakini mpira wake kwa kichwa uliokolewa na Wilbol Maseke. Kwa mara hii, kona haikuwa ya Faida kwa Prisons.
Dakika ya 61 KMC walifanya mabadiliko matatu kwa mpigo, Deogratius Kulwa nafasi ya Awesu Awesu, Ismail Gambo nafasi ya Twalib Nuru na Rashid Chambo Nafasi ya Tepsie Evance. Haya ni mabadiliko ya kiufundi yalikuwa huku kila nafasi ikiwa na mbadala wake ili kuongeza kasi mpya.
KMC waliongeza kasi ya mashambulizi dakika ya 69, Rashid Chambo aliingia na mpira kwenye eneo la goli la Prison na kutoa pasi nzuri kwa Ibrahim Elias, lakini shuti lake lilipaa juu ya lango.
Prisons walifanya mabadiliko ya kiufundi dakika ya 74 kwa kumuingiza Beno Ngassa na kummtoa Edwin Balua. Dakika ya 76, Freddy Tangalo almanasura aisawazishie timu yake lakini shuti lake liliokolewa kiustadi kabisa na Yona Amos. Yona Amos alikuwa kwenye kiwango bora sana leo.
Yona Amos anapewa kadi ya Njano dakika ya 80 kwa kile muamuzi alichokitafsiri kama kuchelewesha Muda. Dakika hizi pia anaingia Daruwesh Saliboko upande wa KMC.
Dakika ya 82, Waziri Junior Shentembo anaisawazishia KMC kwa kichwa akimalizia krosi murua kutoka Rashid Chambo. 1-1 kwenye ubao.
Dakika 4 za nyongeza kukamilisha dakika 90 za mchezo. Prisons wanammtoa Zabona Mayombya na Kumuingiza Mussa Haji
Kila mtu alionekana kuutaka mchezo. Mwalimu Moalin alicheza na mfumo wa 4-2-3-1, akiwa na Waziri Junior kama mshambuliaji pekee akipokea huduma kutoka kwa viungo wa tatu nyuma yake. Tepsie Evance, Awesu Awesu na Ibrahim Elias. Ila ushindani mkubwa ulikuwa kwenye eneo la Kiungo cha kati, Freddy Tangalo na Issah Ndala walipapatuana vilivyo na Omary Abdallah na Joshua Nyantini.
Prisons walicheza kinidhamu sana wakiiheshimu KMC. Aicheza na mfumo wa 4-4-2, akitegemea mbio za mawinga wake Zabona Mayombya na Edwin Balua kwenye Kushuka kusaidia ulinzi wakati hawana mpira. Huku juu ya walinzi, muda mwingi Omary Abdallah alikuwa hatoki, zaidi Nyantini ndiye alikuwa akiunganika na safu ya ushambuliaji. Jeremiah Juma na Batshie walicheza kama washambuliaji.
Mchezo ulimalizaka kwa 1-1. Matokeo sawia kabisa kwa mchezo ambao ulikuwa 50-50.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...