Mchambuzi wa soka nchini Gharib Mzinga amesema Simba inatakiwa kufanyika maboresho kwenye kikosi chao ili iweze kufika fainali ua CAF Champions League.
Michuano ya AFL imefikia hatua ya nusu fainali baada ya michezo ya robo fainali kumalizika, timu zilizofuzu kwenda hatua ya nusu fainali ni Mamelodi Sundowns, Al Ahly, Esperance de Tunis na Wydad Casablanca. Al Ahly itakutana na Mamelod Sundowns huku Wydad AC ikikutana na Esperance, michezo yote ikipigwa siku ya jumapili. Michuano hii ipo chini ya Shirikisho la soka Duniani FIFA, michuano ambayo ilikuwa inashirikisha jumla ya timu nane (8).
Klabu ya Simba ilipata nafasi ya kushiriki katika michuano mikubwa ya African Football League na ikapangwa kuanza na Al Ahly katika mchezo wa robo fainali na ikaondoshwa kwa faida ya goli la ugenini baada ya kufungana 2-2 katika uwanja wake wa nyumbani, Benjamin Mkapa na kutoka sare ya 1-1 ugenini, Cairo Stadium.
Baada ya Simba kuondoshwa mchambuzi wa michezo nchini Gharibu Mzinga ametoa tathmini yake juu ya kile ambacho Simba imekipata kutokana na ushiriki wake katika michuano hii, Mzinga amesema hii itawafanya Simba waongeze kujiamini zaidi kuelekea katika michuano ya Ligi ya mabingwa, Mzinga amesema kwa aina ya kikosi walichonacho hawawezi kufika fainali ya michuano hiyo labda itokee tu kama bahati.
Simba wameimarika, wamepunguza presha waliyokuwa nayo misimu kadhaa nyuma, utakumbuka waliwahi kufungwa magoli matano na Al Ahly,……… kama unaenda Cairo kucheza na Al Ahly na unawabana mbavu, na uliwambana mbavu nyumbani inaonyesha kwamba kikosi chao kinaimarika.
Kutolewa ni kesi nyingine, ili uende hatua inayofuata lazima uwe na kiwango bora zaidi ya hiyo ambayo uko nayo,…. Simba aina ya kikosi ambacho wako nacho, timu ambayo wako nayo haina nguvu ya kucheza fainali ya CAF Champions League, haimaanishi kwamba haiwezi kwenda, inaweza ikaenda lakini sio kwenye ngazi ya ‘Concistency’, sio kwenye daraja la kwenda mara kwa mara hiyo inakuwa kama bahati tu.