FC Barcelona imeanzishwa mwaka 1899 na Real Madrid ilianzishwa miaka mitatu baadae yaani 1902. Baada ya mwaka mmoja mbele El Classico ya kwanza ikapigwa baina ya timu hizi mbili, Ilikuwa sehemu ya michuano isiyo rasmi ya Copa de la Coronacion. Mchezo mwingine mkubwa uliozihusisha timu hizi mbili ulikuwa ni wa kirafiki wakati huo Laliga ilikuwa haijaanzishwa na michuano mikubwa ilikuwa ya Copa de Espana.
Baada ya muda kupita timu hizi zimekuwa zikikutana mara kwa mara hasa baada ya kuanzishwa kwa kwa ligi ya Laliga mwaka 1929.
Mechi hii iliongeza uhasama zaidi baada ya vita iliyohusisha usajili wa nyota Alfredo de Stefano mwaka 1950 na maamuzi yenye utata pindi timu hizi zilipokuwa zikikutana. Timu hizi pia zilitoa wanasoka bora zaidi Duniani kama Ladislao Kubala na Luis Suarez kwa Barcelona huku Real Madrid wakiwatoa watu kama Ferenc Puskas na Di Stefano.
Mchezo wa kukumbukwa zaidi kwa timu hizi mbili ni ule uliopigwa mwaka 1974, kipindi hicho Johan Cruyff akiwa kwenye ubora wake, Barcelona ilishinda goli 0-5 ikiwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, huo pia unasemwa kama mchezo bora zaidi kwa nyota huyo ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo.
Kwa kizazi cha hivi karibuni msimu wa mwaka 1994, kipindi hicho Johan Cruyff akiwa kocha Barcelona waliibuka na ushindi wa goli 5-0 kipindi ambacho Romario akiwa katika ubora wake, haya ndio matokeo yenye umaarufu mkubwa zaidi.
Mwaka uliofuata Real Madrid pia ililipa kisasa ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Santiago Bernabeu kwa kuichapa goli 5-0 Barcelona.
Mwaka 2011, Barcelona ikiwa chini ya Pep Guardiola waliiangushia nyundo nzito tena Real Madrid (5-0) ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa chici ya Kocha Jose Morinho, msimu wa 2018, Barca walifanya hivyo tena (5-0) kipindi ambacho ilikuwa chini ya Ernesto Valverde wakati Real Madrid ikiwa chini ya Julen Lopetegui.
El Classico imebebwa na pia na matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea yakizihusisha timu hizi mbili ikiwemo uhamisho wa wachezaji muhimu kutoka timu moja kwenda nyingine, mfano Bernd Schuster, Michael Laudrup na Luis Figo ambao waliondoka Barca na kujiunga na Real Madrid. Pia Barca iliwahi kufanya usajili katili kwa Real Madrid kama vile Luis Enrique au Samuel Eto’o.
Misimu kadhaa iliyopita El Classico ilikuwa imebebwa na nyota wawili, Cristiano Ronaldo (Real Madrid) na Leonel Messi (Barcelona).
FC Barcelona itashuka dimbani hii leo kuikabili Real Madrid katika dimba lake la nyumbani la Estadi Olympic Lluis Companys ambalo wanalitumia kwa sasa. Hii inakuwa El Classico ya kwanza kwa msimu wa 2023/24.
17:15 Barcelona vs Real Madrid.
UWANJA: Olympic Lluis Companys.
Mwamuzi: Jesus Gil
Zifuatazo ni takwimu za timu hizi mbili kuelekea katika mchezo huo mkubwa hii leo Duniani.
- Real Madrid imeshinda michezo 102.
- Barcelona imeshinda michezo 100.
- Sare 52.
- Barcelona imefunga magoli 415.
- Real Madrid imefunga magoli 424.
- Barcelona imeshinda michezo 63 ikiwa nyumbani.
- Real Madrid imeshinda michezo 65 ikiwa nyumbani.
- Real Madrid imecheza michezo 10 ina alama 25, katika nafasi ya pili (2)
- Michezo mitano ya mwisho ya Real Madrid imeshinda minne (4), imetoa sare mmoja (1).
- Barcelona imecheza michezo 10 ina alama 24 katika nafasi ya tatu (3).
- Michezo mitano (5) ya mwisho ya Barca, imeshinda minne (4), imetoa sare moja (1).
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...