Connect with us

African Football League

MZINGA: MAMELODI ANAINYANYASA AL AHLY.

Mchambuzi wa soka nchini Gharib Mzinga ametoa tathimini yake kuelekea mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Mamelodi dhidi ya Al ahly leo.

Mchezo unaoikutanisha Mamelodi Sundowns dhidi ya Al Ahly umekuwa ni mchezo unaovuta hisia za wapenzi wengi wa soka Barani Afrika, kwa kipindi cha hivi karibuni umekuwa miongoni mwa michezo bora sana.

Leo saa 10:00 Jioni timu hizi mbili zitakutana katika michuano ya African Football League katika hatua ya Nusu Fainali, Mamelodi Sundowns itakuwa ikimkaribisha Al Ahly katika dimba la Loftus Versfeld nchini Afrika Kusini.

Kuelekea katika mchezo huu mchambuzi wa soka Barani Afrika Gharib Mzinga amesema kwa kipindi cha hivi karibuni Mamelodi Sundowns amekuwa akimuonea Al Ahly, hakuna timu yoyote ambayo ina nguvu ya kumnyanyasa Al Ahly Afrika zaidi ya Mamelodi Sundowns.

Hiyo ni African Derby, mechi yenye mvuto zaidi wa football kwa ngazi ya klabu Afrika ni Mamelodi na Al Ahly. Ukiangalia Trend Mamelodi amekuwa akimuonea Al Ahly kwa miaka ya hivi karibuni……… Hakuna timu yoyote Afrika hii, ukiacha Mamelodi Sundowns ambayo ina nguvu ya kumnyanyasa Al Ahly kama anavyofanya Mamelodi.

Al Ahly ni Godfather, ni klabu kubwa zaidi Afrika ambaye ana mpiga kila mmoja anayekuja mbele yake, sasa anapotokea mpinzani ambaye anaonyesha nguvu kubwa ya misuli na kumnyanyasa Al Ahly basi hiyo mechi ina wavutia watu wengi, ndio kinachotokea Al Ahly ana nyanyaswa na Mamelodi Sundowns.

Msimu uliopita mabao matano (5), msimu wa mwaka juzi pia alifungwa mabao matano (5), mwaka jana sare ya 2-2 ndio yalikuwa mazuri kwao, tofauti na hapo wamekuwa wakifungwa, Mamelodi ndio timu pekee ambayo imemfunga Al Ahly Cairo kwenye uwanja mgumu kupata matokeo…….. hiyo ina chagiza mchezo huo kuwa special kwasababu yule Godfather anakutana na Mbabe wake.

Kuiita African Derby kwasababu inahusisha timu mbili kutoka kanda mbili tofauti za mpira.

Gharib Mzinga akizungumza kuelekea mchezo wa leo wa nusu fainali ya AFL kati ya Mamelodi dhidi ya A Ahly.

Mara ya mwisho Al Ahly kupata ushindi mbele ya Mamelodi Sundowns ilikuwa May 15, 2021 katika uwanja wa Cairo International waliposhinda 2-0, imepita michezo mitano (5) bila kupata ushindi, akipoteza tatu (3) na kutoa sare mbili (2).

Hadi hivi sasa Timu hizi mbili zimekutana mara 14 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika tangu 2001, Mamelodi Sundowns imeshina mara nne (4) na Al Ahly imeshinda mara tano (5) na kutoa sare tano (5). Katika michezo sita (6) ya mwisho Al Ahly ameshinda mchezo mmoja (1), Mamelodi Sundowns imeshinda michezo mitatu (3), zimetoka sare mara mbili (2).

Al Ahly haijawahi kupata ushindi kwenye uwanja wa Loftus Versfeld, wamecheza michezo saba (7) ametoa sare nne (4) na kupoteza tatu (3). Mchezo wa mwisho timu hizi kukutana katika uwanja huu Mamelodi Sundowns ilishinda goli 5-2, ilikuwa March 11, 2023.

Makala Nyingine

More in African Football League