Connect with us

International Football

FIFA YAMFUNGIA RAIS WA ZAMANI WA HISPANIA.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Duniani FIFA imefanya uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi.

Shirikisho la soka Duniani FIFA kupitia kamati yake ya nidhamu, leo limemfungia Rais wa zamani wa shirikisho la soka nchini Hispania Luis Rubiales kujihusisha na soka kwa miaka mitatu (3), baada ya kujiridhisha na uchunguzi waliokuwa wanaufanya kuhusu tukio lililosemwa la unyanyasaji.

Hii inakuja baada ya tukio la kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya Taifa ya Hispania, Jenni Hermoso wakati wa utoaji wa tuzo kwenye fainali ya kombe la Dunia kwa wanawake ambazo zilifanyika Sydney, Australia mapema mwaka huu. Timu ya Taifa ya Hispania iliibuka na ubingwa mbele ya England.

Makala Nyingine

More in International Football