Connect with us

Top Story

WAJUMBE UBUNGO WAGOMEA UCHAGUZI.

Wajumbe wa Chama cha soka Wilaya ya Ubongo wamegomea uchaguzi baada ya wagombea wengine majina yao kukatwa.

Wajumbe wa Chama cha soka Wilaya ya Ubungo [UFA] wametangaza kugomea kushiriki uchaguzi kwa kile wanachodai ni ukiukwaji wa utaratibu wa uchaguzi

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wajumbe hao wamedai mchakato wa kupendekeza majina ya wagombea una mashaka baada ya majina ya baadhi ya wagombea kukatwa na kuachwa jina moja kwenye kila nafasi .

Wagombea nafasi ya mwenyekiti walikuwa wanne (4) lakini watatu wamekatwa limebaki jina moja , wagombea nafasi ya ujumbe walikuwa watano ,wanne wamekatwa amebaki mmoja.

Ubungo kilio chetu ni watu waliorudishwa ,aliyerudishwa kwenye nafasi ya Mwenyekiti cheo bado anacho na hajajiuzulu cheo chake, maana yake tutakapomaliza uchaguzi huu tunakazi ya kurudia uchaguzi wa makamu mwenyekiti , hapa sasa kazi yetu itakuwa ni kurudia uchaguzi kila wakati.

Ombi letu kawa DRFA kama watashindwa waturudishie sisi wenyewe maana huyo anayegombea ndio katengeneza kamati ya uchaguzi ,kwanini atengeneze yeye kamati wakati yeye ni mgombea ?

Hapa unajiuliza tunachagua au tunateua , tumeletewa picha tuchague mtu mmoja

Hassan Pazi , kiongozi wa Sifa UTD ya Manzese.

Makala Nyingine

More in Top Story