
Mashujaa wanapoteza mchezo wao wa kwanza wakiwa nyumbani msimu huu kwa kukubali kichapo cha 3-0 mbele ya Azam FC ambao walikuwa kwenye kiwango bora sana hii leo na kuvunja mwiko wa Mashujaa kufungwa kwao Lake Tanganyika. Ushindi huu unawarejesha azam kwenye nafasi yao ya 3 wakifikisha alama 16 baada ya michezo 8.
Mashujaa walionekana kujiamini zaidi wakiwa nyumbani dakika za mwanzo wa mchezo wakichezea mpira na kujaribu kutengeneza nafasi za kujipatia goli la mapema lakini safu ya ulinzi chini ya Daniel Amoah na Edward Manyama ilikuwa imara kummlinda golikipa wao Ahamada.
Kikosi cha Azam kikiwa na muundo tofauti leo na wachezaji wengi kuanza ambao hawakuanza kwenye mchezo uliopita, wakicheza 4-4-2, walijibu mapigo na kuuchukua mchezo huku wakipeleka mashambulizi mfululizo kupitia kwa Djibrill Sillah upande wa Kulia na Kipre Jr upande wa kushoto.
Wakimiliki mchezo kwa 65%, Azam walidhani wamepata goli dakika ya 24 baada mpira wa Feisal Salum kugonga nguzo ya pembeni na kurudi uwanjani akiunganisha kazi nzuri ya Sillah kutokea upande wa kulia.
Azam bado waliendelea kulisakama lango la Mashujapindi a lakini walikaa imara huku na wao wakifanya majaribio kadhaa ya kushitukiza. Lakini hayakummpa tabu sana Ahamada. Wakatai huu wakijisahau kufanya majukumu ya kiulinzi, ilimmlazimu Baraka Mtuwi kufanya kazi ya ziada kuzuia krosi iliyokuwa ikielekezwa kwa Feisal Salum wakati Azam wakijibu shambulizi na kuifanya iwe kona.
Pamoja na kufika sana kwenye eneo la goli la Mashujaa na kuumiliki mpira lakini bado Azam hawakuweza kutumia nafasi zao na mpaka kwenda mapumziko wakiwa 0-0.
Kipindi cha pili kilirejea kwa timu zote kuwa kwenye mawindo ya goli la kwanza na wakishambuliana kwa kupokezana, lakini dakika ya 52, Kipre Jr aliifungulia Azam akaunti ya mabao akiunganisha kwa mtindo wa aina yake krosi maridhawa kutoka kwa Djibrill Sillah. Sillah alikuwa peke yake kwenye eneo la hatari la Mashujaa baada ya awali kuchezewa madhambi kwenye eneo hilo, mpira wa haraka haraka waliouanza Mashujaa ukatoka nje na kuwa mpira wa kurushwa na kurushwa kwa Sillah aliyepiga krosi hiyo bila ajizi akiwa bila bugudha yoyote. Watajilaumu wenyewe Mashujaa.
Dakika ya 68, Djibril Sillah ambaye alionekana kuwa kwenye kiwango bora sana leo, aliipatia Azam bao la pili kwa kufunga goli maridadi kabisa akiuzungusha mpira kwenye nyavu ndogo za juu huku watu wakiamini umetoka baada ya kupenya kwenye nyavu. Alipokea pasi safi kutoka kwa Feisal Salum na bila ajizi akafunga bao tamu sana. 2-0 Azam.
Azam wakafanya mabadiliko kwa kummtoa Idriss Mbombo na kumuingiza Aliassane Diao na haikummchukua muda kuiandikia Azam bao la tatu. Alikuwa ni Feisal salum tena akipiga pasi elekezi kwa mfungaji ambaye alijitoa muhanga kuingiza kichwa kwenye mpira wa 50-50 na kufunga bao. Dakika ya 72, 3-0 Azam
Dakika ya 72 Azam wafanya mabadiliko tena kwa kuwaingiza Iddy Selemani “Nado” na Abdul Suleiman Sopu badala ya Kipre Jr na Feisal Salum na dakika ya 78 wakiwaingiza Yannick Bangala na Ayoub Lyanga nafasi za Djibril Sillah na Yahya Zaid.
Azam waliamua kuupoza mchezo ambao ulionekana wameumiliki kwa asilimia kubwa. Mashujaa walikuwa wameshapooza kwa dakika hizi za mwisho wa mchezo. Mpaka mpira unamalizika Mashujaa 0-3 Azam Fc.

Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 1 year agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 1 year agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 12 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 12 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 1 year agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...