Connect with us

Betting Tips

MKEKA POINT

Wagonga Nyundo wa London wanakutana Washika Bunduki wa Huko huko London kwenye mpambano wa kombe la ligi, Carabao Cup raundi ya 4 baada ya wote kupata ushindi mwembamba kwenye raundi ya 3.

West Ham wameshinda mechi 1 tu kati ya michezo 5 waliyocheza hivi karibuni huku Arsenal ameshinda mechi 3, iktoka sare 1 na kufungwa 1 kwenye mechi zake 5 pia. Haijawahi kuwa mechi rahisi wanapokutana wana London hawa haijalishi nani ana msimu bora zaidi ya mwenzake.

Uwezekano wa wote kupata magoli na mechi kuwa na magoli zaidi ya 2.5 ni mkubwa pia, huku Arsenal akipewa nafasi kubwa ya kushinda mechi hii.

TIP : ARSENAL USHINDI NA MAGOLI ZAIDI YA 2.5

Mabingwa watetezi  wa EFL Cup, Manchester United  wanakutana na wanafainali wa michuano hiyo kwenye mechi ya kisasi mapema sana raundi hii ya 4 huku United akitinga raundi hii baada ya kuwachapa Crystal Palace 3-0 na Newcastle wakimmtoa City kwa ushindi wa 1-0.

United huonekana kuwa makini sana kwenye makombe kama haya, licha ya kutokuwa na muendelezo mzuri wa matokeo kwenye michuano mingine, wakishinda mechi 3 kwenye michezo yao 5 ya mwisho. Lakini wana kibarua kigumu sana mbele Newcastle ambao wana safu nzuri ya kushambulia wakifunga magoli 12 kwenye michezo 5 ya mwisho.

Magoli uhakika kwenye mchezo huu kwa United imeruhusu magoli 8 kwenye michezo 5 ya mwisho lakini na wao wanafunga.

TIP : WOTE KUFUNGANA(BOTH TEAMS TO SCORE)

Udinese hawana ushindi hata mmoja kwenye michezo yao 5 ya mwisho. Wametoa sare 5. Ni mchezo mmoja tu ulioisha na magoli zaidi ya 2.5.

Cagliari wameruhusu nyavu zao kuguswa kwenye michezo 4 kati ya 5. Wameruhusu magoli 15 na kufunga magoli 8 tu. Wameshinda mchezo 1 na kufungwa mitatu(3).

Timu zote hazina matokeo mazuri sana lakini wanakuhakikishia kufungana.

TIP : MAGOLI ZAIDI YA 2.5

Makala Nyingine

More in Betting Tips