Connect with us

Manchester United

ONANA KUIKACHA MAN UNITED JANUARI

Golikipa wa Manchester United Andre Onana atakosa mechi kadhaa muhimu za Manchester United baada ya kuamua kujiunga na wachezaji wenzake wa Cameroon katika michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi Januari

Inafahamika kuwa Golikipa huyo wa zamani wa Inter Millan alikuwa ameachana na soka la kimataifa baada ya kutofautiana na kocha mkuu wa Cameroon Rigobert Song na kusababisha kuondolewa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia la 2022 katikati ya michuano hiyo nchini Qatar. Hata hivyo, wawili hao wamerekebisha tofauti zao na Onana akarejeshwa kwenye timu ya taifa. Kufuatia kurejea kwake alionekana kwenye mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Burundi mnamo Septemba na pia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Senegal wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Oktoba. Onana amekubali kurudi kuichezea timu yake ya Cameroon (The Indomitable Lions) katika michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza Januari 13 nchini Ivory Coast.

Iwapo Cameroon watatinga katika hatua ya fainali, United italazimika kucheza bila huduma ya Onana katika mechi nne za Ligi Kuu, mechi mbili za Kombe la FA na nusu fainali ambayo huenda ikawa ya Kombe la Carabao. Onana amekuwa akiichezea klabu yake mpya hatua kwa hatua na kuibuka shujaa katika ushindi mwembamba wa United kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Copenhagen wiki iliyopita, baada ya kuokoa penati dakika za majeruhi na hivyo kufikisha pointi tatu. Alikuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vyema kwenye mechi ya derby ya 3-0 dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita

Ikiwa Onana ataitikia wito wa kocha wake wa timu ya Taifa, basi United italazimika kumtegemea Altay Bayindir, mlinda mlango wa Uturuki aliyesajiliwa kutoka Fenerbahce wakati wa majira ya joto. Hata hivyo, kwa muda mfupi, Onana ataendelea kusimama katikati ya milingoti mitatu ya United watakapowakaribisha Newcastle United kwenye Kombe la Carabao siku ya Jumatano, kabla ya kumenyana na Fulham kwenye Ligi Kuu ya nchini Uingereza (EPL) siku ya Jumamosi.

Makala Nyingine

More in Manchester United