Connect with us

NBC Premier League

SINGIDA BS, IHEFU WATUNISHIANA MISULI

Singida BS na Ihefu wametoshana nguvu kwenye mchezo uliokuwa na upinzani wa hali juu na uliosheheni wachezaji wengi wa madaraja uliopigwa kwenye dimba la Liti, Singida kwa kufungana 2-2.

Walikua ni Ihefu walioanza kupata bao kupitia kwa Ismail Mgunda dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliochongwa kiustadi na Never Tigere.

Japo mchezo ulionekana wakiutawala sana Ihefu kwa dakika hizi lakini Singida walibadilisha kibao kwa dakika 15 za mwisho kuelekea mapumziko. Dakika ya 31, Habibu Kyombo aliisawazishia timu yake baada ya mabeki wa Ihefu kushindwa kuondoa mpira uliokuwa ukizengea golini kwao.

Dakika ya 38, mshambuliaji Ismail Mgunda alipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikichukuliwa na Jaffary Kibaya.

Alikuwa ni Habibu Kyombo tena, dakika ya 41 akiwaadhibu mabeki wa Ihefu kwa uzembe wao kushindwa kuokoa vizuri mipira ya juu. Akipiga kichwa kutokana na krosi iliyochongwa na Kevin Kijiri.

Mpaka mapumziko Singida BS 2-1 Ihefu.

Kipindi cha pili kilirudi na kasi kama kipindi cha kwanza lakini Ihefu walionyesha dhati zaidi ya kutafuta alama walahu 1.

Jaffary Kibaya akionekana kuwa msumbufu zaidi kwa walinzi wa Singida BS, na mara kadhaa aliwalazimisha kufanya makosa. Azizi Aandambwile alionekana kuzidiwa kwenye eneo la kiungo kutokana an Bruno kutotoa usaidizi mkubwa kwenye ukabaji, Singida wakicheza 4-4-2.

Dakika ya 70, Kibaya alipokea pasi tamu iliyopigwa kutoka katikati ya uwanja, na kumuhadaa golikipa Beno Kakolanya kabla ya kumuhadaa tena Makame na kupasia mpira kwenye goli tupu. 2-2.

Singida BS walijaribu kujipapatua kutafuta alama 3 nyumbani lakini hali ilikuwa ngumu, Ihefu wakiridhika na alama 1 waliimarisha safu yao ya ulinzi kwa kumuingiza Paul Godfrey, nafasi ya Rashid Juma.

Mpaka Muamuzi  Shomari  Lawi anapuliza kipyenga cha mwisho kumaliza dakika zote 90, sio Singida BS wala Ihefu waliotoka kifua mbele.

Singida Big Stars wanafikisha alama 9 na Ihefu wanafikisha alama 8 baada ya michezo 8

Makala Nyingine

More in NBC Premier League