Michezo ya nusu fainali ya pili ya michuano ya African Football league inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili kupigwa. Mamelodi Sundowns ipo nchini Misri kuikabili Al Ahly katika dimba la Cairo International, Esperance watakuwa nyumbani Tunisia kupambana na Wydad Casablanca.
18:00 Esperance de Tunis vs Wydad Casablanca (Agg; 0-1).
- Kwenye michuano hii timu hizi zimekutana mara moja (1), mchezo ambao Wydad alishinda 1-0 akiwa nyumbani.
- Katika mashindano haya timu hizi zimekutana mara nane (8) mara saba (7) mchezo ulimalizika na mara moja (1) mchezo haukumalizika.
- Kwenye michezo saba (7), Esperance imeshinda mara mbili (2), Wydad AC imeshinda mara moja (1) na sare nne (4).
- Mchezo ambao haukumalizika ulikuwa ni mchezo wa pili wa fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika August 17, 2019 baada ya VAR kuzima dakika takribani ya 60 hivi wakati Esperance ikiwa inaongoza goli 1-0.
- Hii ni moja ya mechi bora sana kati ya zile zitakazopigwa hii leo.
21:00 Al Ahly vs Mamelodi Sundowns (Agg. 0-1).
- Timu hizi zimekutana mara moja katika mashindano haya ya AFL, Mamelodi Sundowns ilishinda mchezo huo
- Kwa kipindi cha hivi karibuni zimekutana mara kumi na moja (11), Mamelodi Sundowns imeshinda mara tano (5) na Al Ahly imeshinda mara tatu (3) na michezo mitatu (3) wametoa sare.
- Timu hizi jumla ziecheza michezo 15, Mamelodi Sundowns imeshinda mara tano (5), Sare mara tano (5) na Al Ahly imeshinda mara tano (5), Mamelodi imeifunga Al Ahly magoli 20 na Al Ahly imeifunga Mamelodi magoli 19.
- Al Ahly haijapata ushindi mbele ya Mamelodi tangu waliposhinda May 15, 2021 wa 2-0 ikiwa nyumbani.
- Kocha wa Al Ahly Koller amekutana na kocha wa Mamelodi Sundowns R. Mokwena mara mbili na katika zote Mokwena ameshinda mara moja (1) na sare moja (1).
- moja ya mechi bora zaidi kuishuhudia hii leo ili kutambua nani anasonga hatua ya fainali ya michuano hii kwa mara ya kwanza.