Connect with us

NBC Premier League

KMC IPO TAYARI KUIACHIA AZAM KOCHA MOALLIN.

Klabu ya KMC imesema haitakuwa na kizuizi chochote kama Azam ikimhitaji kocha wao Abdi Hamid Moallin.

Baada ya kuibuka tetesi zinazoihusisha klabu ya Azam FC kuwa kwenye mpango wa kutaka kumrudisha kocha wao wa zamani Abdi Hamid Moallin kufuatia kufanya vizuri akiwa na KMC, Mtendaji Mkuu wa KMC Daniel Mwakasungula amesema hakuna taarifa yoyote waliyopokea kutoka kwa kocha wao juu ya tetesi zinazoendelea.

Sisi pia tunasikia na kuona kama ambavyo nyie mnasikia na kuona kupitia mitandao, mwalimu Moallin bado ana mkataba na KMC FC kwa hiyo kinachoendelea ni kwa sababu ameonesha uwezo mkubwa kwa hiyo hizo taarifa lazima ziwepo.

Hadi sasa kila kitu bado ni tetesi na mwalimu hajasema chochote, tunachojua sisi mwalimu anaendelea na majukumu yake kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazokuja za Ligi Kuu ya NBC.

Kama itatokea atatupa taarifa rasmi ya ofa aliyopata kutoka klabu nyingine hilo ni jambo jingine, lakini huwezi kumzuia mtu anapotaka kuondoka kwa sababu zake binafsi inabidi uheshimu.

Kwa ninavyomfahamu Moallin ni kocha mwenye weledi, msikivu na tayari alishakubali na kuendana na mazingira ya KMC FC, anafurahia maisha ya Kinondoni. Mwisho wa siku akiamua kuondoka tutaheshimu uamuzi wake.

Mtendaji mkuu wa klabu ya KMC, Daniel Mwakasungula.

Inaelezwa kuwa, Azam FC ipo katika mpango wa kumrudisha Moallin Chamazi na tayari imefanya majaribio kadhaa lakini kocha huyo amepiga chini na ofa ya mwisho iliyotumwa na Azam kwa Moallin ni kiasi cha Tsh. 250 ili kumng’oa KMC lakini kocha huyo anaeamini katika vijana bado hajaijibu!

Makala Nyingine

More in NBC Premier League