Winga wa Tottenham, Dejan Kulusevski ameeleza jinsi soka la ngazi ya chini linavyosaidia katika kuzalisha nyota wajao wa mchezo huo, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden akizungumzia umuhimu wa watu wa kuigwa katika tamasha maalum la UEFA Grassroots Festival of Football, linaloendeshwa na EA SPORTS FC
Kulusevski, ambaye ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji mahiri wanaocheza katika eneo la mbele katika ligi kuu ya nchini Uingereza (EPL), alianza maisha yake ya ujana na IF Brommapojkarna, akitumia miaka 10 na klabu hiyo yenye maskani yake Stockholm kabla ya kuhamia Serie A na Atalanta mnamo 2016.
Ili kuwa mzuri katika soka, lazima ucheze kila siku, siku nzima. Ukiwa na marafiki zako, wachezaji-wenza, cheza tu kadri uwezavyo na ufurahie. Siku zote hiyo ndiyo kanuni nambari 1 katika soka – usisahau kujiburudisha. Popote ulipo, unahitaji tu mpira kucheza mpira. Huo ndio mchezo mzuri zaidi ulimwenguni.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Grimsta IP, nyumbani kwa Brommapojkarna, nyota huyo wa Spurs alisema.
Tamasha la UEFA Grassroots la Soka linaendeshwa na EA SPORTS FC, chini ya mpango wa EA SPORTS FC FUTURES, kwa lengo la kukuza soka katika ngazi ya mashinano.
Tukio hili linasimamiwa na EA SPORTS, huku wachezaji wachanga kutoka shule na vilabu vya eneo hilo wakishiriki katika shughuli ikiwa ni pamoja na michezo ya pande ndogo, changamoto za ujuzi zinazotolewa na maktaba ya mafunzo ya kidijitali ya EA SPORTS FC FUTURES.
Bila shaka ni muhimu. Kila mtoto anataka kucheza mpira, kila mtu anataka kuwa mfano kwa jamii. Nilipokuwa mdogo mambo haya hayakuwepo lakini nilikuwa na watu ambao nilikuwa nawatazama, watu wakubwa ambao walitutunza na kucheza mpira nasi. Nina furaha kuwa hapa, kusaidia watoto, kucheza nao mpira na kujibu maswali yao.
Kulusevski alijibu alipoulizwa kuhusu umuhimu wa mipango kama vile EA SPORTS FC FUTURES kwa maendeleo ya soka kuanzia ngazi ya chini (vijana).