Connect with us

Betting Tips

MKEKA POINT

Ajax hawana msimu wa kuvutia sana kwani hata kwenye michezo yao 5 iliyopita hawajashinda hata mechi 1 huku wakifungwa mara 4 na sare 1 tu. Hawana wastani mzuri wa kufunga mabao kwani wana goli 7 tu za kufunga huku wakiruhusu 14 langoni kwao. Ni mechi 3 tu za kwao zimeisha zaidi ya magoli 2.5 kwenye mechi 5 za mwisho.

Volendam upande wao wana 0 kwenye tofauti ya magoli, wakifunga 8 na kuruhusu 8. Hawana wastani mzuri wa kushinda pia lakini mechi zao hivi karibuni nyingi zimeisha kwa timu zote kufungana(YGG-4, NGG-1)

DONDOO: MAGOLI ZAIDI YA 2.5

Torino na Frosinone wanafanana kwenye vitu vingi katika mechi zao 5 za mwisho. Wote wameshinda mchezo mmoja, sare 1 na kupoteza mara 3. Torino anatarajiwa kushinda mechi hii japo haitokuwa rahisi.

Frosinone wamefunga mabao 7 kwenye mechi 5 za mwisho lakini pia wameruhusu mabao 10. Torino upande wao wamefunga goli 1 tu. Wote wanaweza kufungana mchezo huu, japokuwa rekodi ya ufungaji upande wa wenyeji hairidhishi sana.

DONDOO: TORINO USHINDI AU TIMU ZOTE KUFUNGANA

Ni rahisi kuipa Valencia leo kwakuwa wanacheza na timu ya daraja la chini, lakini michuano hii imekuwaga na kawaida ya kutoa matokeo ya kushangaza. UD Logrones inaweza kuwa timu ya Segunda, lakini inatamba sana pande zake kuliko Valencia pande zake. Wakipata ushindi kwenye mechi 4 kati ya 5 za mwisho na kupoteza mmoja tu, Logrones wanaweza kuwapa mshituko Valencia waliopata ushindi mmoja tu kwenye michezo ya 5 ya mwisho.

Wote wanaruhusu kufungwa kwenye mechi zao hata kama wakishinda lakini Logrones kafunga mabao 15, mara 3 ya magoli ya Valencia kwenye mechi 5 za hivi karibuni. Ni mechi ambayo inaweza ikakupa magoli mengi leo.

DONDOO : VALENCIA USHINDI

Makala Nyingine

More in Betting Tips