Connect with us

African Football League

FAINALI AFL KUPIGWA JUMAPILI NOVEMBER 5.

Hii ni fainali ya kihistoria Jumapili hii kati ya wababe Wydad Athletic Club na Mamelod Sundowns.

Mchezo wa kwanza wa fainali ya African Football League utapigwa jumapili, November 5 katika Dimba la Mohamed V lililopo Casablanca nchini Morocco kwa kuwakutanisha mwenyeji Wydad AC na Mamelodi Sundowns kutoka nchini Afrika Kusini.

Tayari Mamelodi Sundowns imeshatua nchini Morocco kwaajili ya mchezo huu mkubwa ambao unabeba historia ya kuwa fainali ya kwanza ya michuano hii mipya kufanyika Barani Afrika. Mchezo wa marejeano unatarajiwa kupigwa November 11 katika dimba la Loftus Versfield lililopo Pretoria nchini Afrika Kusini.

Mamelodi imefika katika hatua hii ya Fainali kwa kuiondosha Petro Atletico de Luanda ya Angola katika hatua ya robo fainali na Al Ahly ya Misri aliyoiondosha katika hatua ya nusu Fainali.

Wydad Athletic Club imefika hatua hii ya fainali kwa kuziondosha Enyimba ya Nigeria katika hatua ya robo fainali na Esperance de Tunis ya Tunisia katika hatua ya nusu fainali.

Makala Nyingine

More in African Football League