Ligi kuu kandanda Tanzania Bara mzunguko wa tisa (9) unatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja vitatu (3) tofauti nchini.
16:00 KMC vs DODOMA JIJI
UWANJA: UHURU STADIUM, DAR ES SALAAM
- KMC itaialika Dodoma Jiji hii leo katika dimba la uhuru ikiwa na mwendelezo bora sana kwa siku za hivi karibun chini ya kocha Abdul Moallin ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Azam fc.
- Katika michezo saba (7) ya mwisho timu hizi kukutana, KMC imeshinda michezo miwili (2) na Dodoma Jiji imeshinda michezo mitano (5).
- Tangu zimeanza kukutana timu hizi hazina historia ya kutoa sare.
- KMC imefunga magoli manne (4) dhidi ya Dodoma Jiji.
- Dodoma Jiji imefunga magoli saba (7) ikiwa ni wastani wa goli moja (1) kwa kila mchezo.
- Mchezo wa mwisho timu hizi kukutana katika uwanja wa uhuru ilikuwa November 15, 2022 na Dodoma ilishinda 1-2.
- KMC ipo nafasi ya nne (4) ya msimamo wa Ligi kwasasa ikiwa na alama 15, imecheza michezo nane (8), imeshinda michezo minne (4), imetoa sare michezi mitatu (3), na kupoteza mchezo mmoja (1), imefunga magoli nane (8) na kuruhusu magoli tisa (9).
- Dodoma Jiji ipo nafasi ya tano (5) ya msimamo wa Ligi kwasasa ikiwa na alama 12, imecheza michezo nane (8), imeshinda michezo mitatu (3), imetoa sare michezo mitatu (3), imepoteza michezo miwili (2), imefunga magoli nane (8) na kuruhusu magoli nane (8).
16:00 MTIBWA SUGAR vs JKT TANZANIA.
UWANJA: MANUNGU COMPLEX, MOROGORO
- Mtibwa Sugar hii leo itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania, hii ni miongoni mwa michezo bora itakayochezwa hii leo, huu utakuwa ni mchezo wa Tatu (3) kwa kocha Zuberi katwila akiwa na kikosi cha Mtibwa, michezo miwili iliyopita amepata ushindi mmoja (1) na kupoteza mchezo mmoja (1).
- Katika michezo saba (7) ya mwisho ambayo timu hizi zimekutana, JKT Tanzania imeshinda mara tatu (3) na Mtibwa Sugar imeshinda mara moja (1), na zimetoka sare mechi tatu (3).
- Mtibwa Sugar imecheza michezo nane (8), iko nafasi ya 16 ya msimamo wa Ligi, imshinda mchezo mmoja (1), imetoa sare michezo miwili (2), imepoteza michezo mitano (5).
- Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani imecheza michezo mitano (5), imeshinda mchezo mmoja (1), imetoa sare mchezo mmoja (1) na kupoteza michezo mitatu (3).
- JKT Tanzania imecheza michezo nane (8), ipo nafasi ya sita (6) ya msimamo wa Ligi, imeshinda michezo mitatu (3), imetoa sare michezo miwili (2) na imepoteza michezo mitatu (3).
- JKT Tanzania ikiwa ugenini imecheza michezo minne (4), imeshinda mchezo mmoja (1), imetoa sare mchezo mmoja (1) na imepoteza mchezo mmoja (1).
- Mchezo wa mwisho kupigwa manungu ulikuwa wa FA, February 26,2021 zilipotoka sare ya 2-2.
19:00 KAGERA SUGAR vs TANZANIA PRISON
UWANJA: KAITABA STADIUM, KAGERA.
- Timu hizi zimekutana mara 16 katika michezo yote, kila timu ikishinda mara nne (4) na sare nane (8), ni miongoni mwa michezo migumu haswa ndani ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika uwanja wa Kaitaba ilikuwa May 14, 2023, ambapo Tanzania Prison iliibuka na ushindi wa goli 0-1.
- Kagera Sugar ipo nafasi ya nane (8) ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa imecheza michezo nane (8), imeshinda michezo miwili (2), imepoteza michezo mitatu (3), imetoa sare michezo mitatu (3).
- Kagera Sugar imecheza michezo mitatu (3) nyumbani, imeshinda mchezo mmoja (1), haijapoteza mchezo wowote, na imetoa sare michezo mitatu (3).
- Tanzania Prison ipo nafasi ya 14 ya msimamo wa Ligi, ikiwa na alama saba (7) katika michezo nane (8) iliyocheza, imeshinda mchezo mmoja (1), imepoteza michezo mitatu (3) na imetoa sare michezo minne (4).
- Tanzania Prison katika Ardhi ya ugenini msimu huu imecheza michezo minne (4), haijapata ushindi wowote, imetoa sare mbili (2), na imepoteza imepoteza michezo miwili (2).
- Tanzania Prison Msimu huu imefungwa magoli 13, imefunga magoli nane (8).
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...