Las Palmas wametoka kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Monacor kwenye michuano ya Copa Del Rey. Wakishika nafasi ya 10 kwenye La Liga huku wakishinda mechi 4 kwenye mechi zao 5 za mwisho, sio timu ya kubeza na hasa ikiwa nyumbani. Kwenye mechi zao wamefunga zaidi ya magoli 2.5 kwenye mechi 4 kati ay 5 za hivi karibuni.
Atletico Madrid wanajua ushindi wa leo utawapeleka hadi nafasi ya 1 kwenye msimamo wakiishusha Real Madrid. Ni mechi watayoitolea sana macho leo. Wametoka kuichapa Alaves 2-1 kwenye muendelezo mzuri wa matokeo yao (U4,S1,F0). Wamefunga magoli 12 kwenye michezo hiyo wakiruhusu 6 tu.
Magoli pasi na shaka kwenye mchezo huu ni mengi, lakini Atletico wanaitaka sana mechi, japo Las Palmas nao sio wanyonge nyumbani na watammpa mechi haswa Diego Simeone.
DONDOO : MAGOLI ZAIDI YA 2.5
Matajiri wa Ufaransa, PSG wamerudi kwenye ubora wao wakifunga magoli 13 kwenye michezo ya 5 ya mwisho, wakipata ushindi mara 4 kwenye michezo hiyo na mara ya mwisho wakipata ushindi ugenini kwa Brest wa 2-3. Wako alama 1 tu nyuma ya vinara wa ligi, Nice na kama watapata ushindi leo watapanda kileleni wakiwasubiri wapinzani wao wateleze.
Montpellier hawana rekodi nzuri sana kwa PSG wakifungwa nao mara 18 na wao wakishinda mara 4 tu dhidi yao. Montpellier wameshinda mechi zao 2 hivi karibuni moja ikiwa ya mwisho dhidi ya Toulouse wakiwachapa 3-0. Wamefunga mabao 8, kuruhusu 4 langoni mwao. Pamoja na yote hatutarajii watakuwa mfupa mgumu sana kwa PSG.
DONDOO : PSG USHINDI
Bologna wanashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Serie A, nafasi moja tu nyuma ya wapinzani wao wa leo Lazio. Wakati Bologna akitoka kummfunga Verona 2-0, Lazio walipata ushindi muhimu dhidi ya Fiorentina. Wote wanaingia wakiwa na morali ya ushindi.
Lazio wanaichungulia nafasi ya 5, wameshinda mechi 4 kati ya 5 za hivi karibuni na 3 kati ya hizo zikiwa na magoli zaidi ya 2.5 na timu zote kufungana. Namba hizo hizo wanazo Bologna isipokuwa tu, wao wamefunga magoli mengi zaidi ya Lazio, 10 dhidi ya 9 na kuruhusu 4 dhidi ya 6.
Kwa matokeo sio rahisi kutabiri lakini magoli nakuhakikishia yatakuwa mengi.
DONDOO : SARE AU TIMU ZOTE KUFUNGANA, MAGOLI ZAIDI YA 2.5