Beki wa Chelsea Thiago Silva yuko kwenye mipango ya kuwa kocha mkuu atakapomaliza maisha yake ya soka. Akiwa na umri wa miaka 39 na mkataba wake Chelsea ukikaribia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, Silva anafikiriwa kukaribia kustaafu mchezo huo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amefurahia maisha mazuri na ya kina akiwa katika kilele cha ubora wa kiwango chake mwa kandanda. Baada ya kukaa Brazil na Urusi, alikaa kwa misimu mitatu kama nyota huko AC Milan, ambapo alishinda taji la Serie A, kabla ya kunyakua mataji saba ya Ligue 1 katika miaka minane huko nchini Ufaransa akiitumikia Paris Saint-Germain. Chelsea ilimnyakua mkongwe huyo mwaka 2020 na anabaki kuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Mauricio Pochettino. Pamoja na mlinda mlango Robert Sanchez, ndiye mchezaji pekee wa Chelsea kucheza kila dakika nyingi katika Ligi Kuu ya nchini Uingereza (EPL) msimu huu.
Wakati anapanga kuendelea kwa angalau msimu mmoja zaidi, anaangalia uwezekano wa kufundisha mara tu atakapoamua kustaafu kazi yake.
Kwenye kiwanja cha mpira tayari mimi ni kocha kidogo, sivyo? Ninapotazama mchezo kutoka nyuma, naona vitu vingi. Na kisha ninawaonya [wengine] kuhusu hali fulani. Ninazungumza na wafanyakazi, na Pochettino, ili tusifanye makosa. Wakati mwingine, ni sisi tu uwanjani tunatambua nini kibaya na nini kinaweza kufanywa vizuri zaidi. Na kuna hali ambazo wale walio nje ya uwanja, kwa akili safi, wanaona vizuri zaidi. Uhusiano huu ni muhimu.
Thiago Silva akizungumza na kituo cha The Guardian kuhusiana na uwezekano wake wa kuwa kocha hapo badae.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil huenda akajumuishwa katika kikosi cha kwanza wakati Chelsea watakapoitembelea Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Ligi Kuu siku ya Jumatatu.